Sunday, August 18

Ugonjwa wa Zinaa wa Kaswende (Syphilis) : Dalili Zake, Madhara Yake Na Jinsi Ya Kujikinga

0


Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Ugonjwa
wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha
madhara mengi. 


Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara
mengi sana kama kujifungua kiumbe mbacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa,
mtoto kupata matatizo wakati wa ukuaji wake, degedege na kuongezeka kwa
vifo vya watoto wachanga nchini. 

Ugonjwa wa kaswende huathiri zaidi ya
mimba millioni moja duniani kote kila mwaka na huchangia theluthi mbili
ya vifo vya watoto wale wanaozaliwa tayari wameshakufa katika nchi za maeneo ya
jangwa la sahara. 

 
 Asilimia 30 ya mimba zinazoathiriwa na kaswende
huishia watoto kufariki wakati wa kuzaliwa. Asilimia nyengine 30 ya
mimba zinazoathiriwa na kaswende husababisha watoto kuzaliwa na ugonjwa
huu wa  kaswende, kupata matatizo ya ukuaji wao, degedege na kuongeza vifo vya
watoto kwa asilimia 50. 

 
Ugonjwa
wa ukimwi na kaswende mara nyingi huambatana pamoja. Ugonjwa wa
kaswende huongeza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa ukimwi.


Visababishi vya ugonjwa wa kaswende

Kama tulivyosema awali, kaswende husababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Njia za maambukizi za ugonjwa huu ni kama zifuatavyo;

 • Kupitia kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeambukizwa kaswende
 • Kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex)
 • Kujamiana kupitia njia ya mdomoni (oral sex)
 • Mama aliyepata ugonjwa wa kaswende wakati wa ujauzito anaweza kumuambukiza mtoto wake wakati wa ujauzito.
 • Kuambukizwa
  kupitia michibuko au mipasuko kwenye ngozi wakati wa kujamiana au
  wakati mwengine wowote pale mtu anapogusana na mtu mwenye kaswende ikiwa
  wote wawili wana mipasuko kwenye sehemu mbalimbali za ngozi zao. Sio
  rahisi mtu kutambua kama ana michibuko au la kwenye ngozi kwani mengine
  inakuwa midogo sana isipokuwa ile ambayo inaweza kuonekana kwa macho.

Dalili na Viashiria vya ugonjwa wa kaswende
Dalili
na viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea na aina ya ugonjwa wa
kaswende wenyewe. Kuna aina tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;

 • Ugonjwa wa kaswende wa awali (Primary syphilis)
 • Ugonjwa wa kaswende wa pili (Secondary syphillis)
 • Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
 • Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
 • Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis)

Kaswende ya awali (primary syphilis)
Dalili
ya kwanza ya aina hii ya kaswende ni kutokea kwa kidonda kidogo cha
mviringo (chancre kama kinavyojulikana kitaalamu) katika sehemu ambayo
bakteria wameingilia na hutokea kati ya siku 10 hadi miezi mitatu (kwa
kawaida kuanzia wiki 2 hadi 6) baada ya mtu kupata maambukizi ya
kaswende. Kidonda hiki kinaweza kutokea kwenye sehemu ya haja kubwa,
shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mdomoni (lips), uume (penis),
ulimi, vulva, tupu ya mwanamke (vagina) na sehemu nyengine mwilini. Tezi
(lymph nodes) ambazo zipo karibu na sehemu iliyotokea kidonda hiki
kawaida huwa zinavimba baada ya siku 7 hadi 10. 

Kidonda hiki
hakiambatani na maumivu na kwa kuwa kinaweza kutokea katika sehemu
zilizojificha kama kwenye shingo ya kizazi, sio rahisi mtu kutambua kama
na aina hii ya kaswende. Kidonda hiki kinaweza kuwepo kwa muda wa wiki 3
hadi 6 kama mtu hatapata tiba na kinatoweka chenyewe bila tiba au baada
ya kupata tiba. 

Robo tatu ya wale ambao hawapati tiba huishia kuingia
kwenye kundi la kaswende ya aina ya pili (Secondary syphilis).

 
Kaswende aina ya pili (Secondary syphilis)
Aina hii hutokea wiki 4 hadi 10 baada ya mtu kupata kaswende ya awali. Dalili za aina hii ya kaswende ni;

 • Vipele
  ambavyo haviwashi katika viganja vya mikono au nyayo za miguu. Vipele
  hivi pia vinaweza kutokea mwili mzima au sehemu mbalimbali za mwili.
 • Uchovu
 • Kuumwa kichwa
 • Homa (fever)
 • Kunyofoka nywele
 • Vidonda vya koo (sore throat)
 • Kuvimba kwa matezi mwili mzima
 • Maumivu ya mifupa (joint pain)
 • Kupungua uzito
Kaswende
ya aina hii inakuwepo kwa wiki kadhaa na hupotea hata bila kupata tiba
kwa mtu aliyeathirika. Pia inaweza kujirudia rudia katika kipindi cha
mwaka mmoja hadi miwili na mtu huingia kwenye kundi la aina ya tatu ya
ugonjwa wa kaswende (latent syphilis) baada ya miaka miwili.

 
Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
Hii
inajulikana kama kaswende ambayo inaweza kuthibika tu kwa kutumia
vipimo vya maabara (serological test). Imegawanyika katika makundi
mawili:

i.
Early latent syphilis (kaswende iliyojificha ya awali) – Hii ni ile
ambayo hutokea ndani ya kipindi cha mwaka mmoja baada ya muathirika
kuugua kaswende aina ya pili (secondary syphilis). Aina hii huwa na
dalili zinazojirudia kama za kaswende ya pili (secondary syphilis)

ii.
Late latent syphilis (kaswende iliyojificha ya kuchelewa) – Hii hutokea
baada ya mwaka mmoja wa kuugua kaswende ya aina ya pili (secondary
syphilis). Wakati wa kuugua aina hii, muathirika anakuwa hana dalili
wala viashiria vyovyote vile na uwezo wake wa kuambukiza mtu mwengine
unakuwa chini au hawezi kabisa kumuambukiza kaswende mtu mwengine.

 
Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
Asilimia
30 ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia
kwenye kundi hili na hutokea miaka 15 – 30 baada ya maambukizi ya
kaswende hapo awali. 

Aina hii inaweza kuathiri viungo kama macho,
ubongo, mishipa ya fahamu (Neurosyphilis), jointi au viunganishi vya
mifupa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu na hivyo kusababisha
madhara makubwa kama;

 • Upofu
 • Magonjwa ya moyo – Aortic dissection type B, syphilitic aortitis
 • Magonjwa ya akili
 • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
 • Mtu kuwa kiziwi
 • Kupungukiwa na kumbukumbu (Memory loss)
 • Kifo

Pia
aina hii ya kaswende inaweza kuathiri mfumo wa chakula (abdominal
organs), mfumo wa kupumua (respiratory system) na mfumo wa uzazi
(reproductive system).

 
Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis)
Aina
hii hutokea wakati wa ujauzito au baada ya mtoto kuzaliwa. Robo mbili
ya wototo wanaozaliwa hawaonyeshi dalili zozote. Nusu ya watoto wenye
maambukizi ya kaswende hufariki muda mfupi kabla ya kuzaliwa au baada ya
kuzaliwa. Dalili za aina hii ya kaswende kwa mtoto mchanga zinaweza
kutokea baada ya kuzaliwa au wiki 2 hadi miezi 3 baada ya kuzaliwa;

 • Kutoongezeka uzito au kushindwa kukua
 • Homa
 • Kukasirika haraka (irritability)
 • Kutochongoka kwa pua, pua inakuwa bapa (no bridge to nose or saddle nose)
 • Vipele kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo
 • Vipele vya rangi ya madini ya shaba kwenye uso, viganja vya mikono na nyayo
 • Vipele kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu ya haja kubwa
 • Kutokwa na majimaji puani
 • Kuongezeka ukubwa wa ini na bandama (hepatosplenomegally)
 • Ngozi kuwa ya njano (jaundice)
 • Upungufu wa damu mwilini (anemia)
Dalili kwa mtoto mkubwa
 • Kuathirika meno (Hutchinson teeth)
 • Maumivu ya mifupa
 • Upofu
 • Kupungua uwezo wa kusikia au mtoto kuwa kiziwi
 • Ukungu kwenye mboni za macho (Clouding of cornea)
 • Vidonda rangi ya kijivu kwenye sehemu ya haja kubwa na kwenye tupu ya mwanamke (vagina)
 • Ngozi kuwa na mabaka meusi kwenye mdomo, sehemu za siri na sehemu za haja kubwa
 • Maumivu kwenye mikono na miguu
 • Kuvimba jointi za mifupa

Ugunduzi wa ugonjwa wa kaswende
Ugunduzi
wa ugonjwa wa kaswende huusisha utambuzi wa dalili na viashiria vya
ugonjwa huu (hii hufanywa na daktari) kupitia historia ya mgonjwa,
vipimo vya damu na vipimo vya kugundua bakteria aina ya Treponema pallidum. 

 
a. Utambuzi wa dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende

 1. Hufanywa na daktari
 2. Huusisha historia ya mgonjwa

b. Vipimo vya damu
Vipimo hivi vinahusisha utambuzi wa chechembe za antibodies dhidhi ya bakteria Treponema pallidum.
Majibu yanaweza kuwa false positive (Wale ambao vipimo vimeonyesha wana
kaswende lakini hawana ugonjwa huu,hii hutokea kwa wale ambao waliugua
kaswende awali na hali hii inaweza kuwepo hadi miezi mitatu baada ya
kupona ugonjwa huu au wale wenye ugonjwa wa kifua kikuu, malaria,
wajawazito, measles, endocarditis, connective tissue disease nk.) au
false negative (Wale ambao wameathirika na kaswende lakini vipimo
vinaonyesha hawana kaswende). Mara nyingi ni vigumu sana kuthibitisha
uwepo wa ugonjwa huu, hivyo vipimo hurudiwa ili kupata uthibitisho.

 • RPR (Rapid plasma reagin) test
 • VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)
 • The microhemagglutination assay [MHA-TP] Hufanywa kuthibitisha ugonjwa wa kaswende
 • Fluorescent-treponemal-antibody
  absorption [FTA-ABS, enzyme-linked immunosorbent assay ELISA]) Hufanywa
  kuthibitisha ugonjwa wa kaswende
 • PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) vya Treponema pallidum.
 • Complete Blood Count – Kipimo cha kuangalia wingi wa damu na aina tofauti za chembechembe za damu

c. Vipimo vya kugundua bakteria
Hufanywa kwa kutumia hadubini ( Dark field microscopy).
d. Vipimo kwa wale wenye madhara ya kaswende

 • Picha ya X-ray ya kifua, uti wa mgongo
 • Vipimo
  vya moyo – ECG, transesophageal echocardiogram,aortic angiography,
  doppler ultrasonography, chest MRI, cardiac CT scan (contrast), CT
  angiography.
 • CT scan ya kichwa, mfumo wa chakula (abdominal CT)
 • MRI ya kichwa, uti wa mgongo, brainstem
 • Bone scan (Vipimo vya mifupa)
 • Vipimo vya macho
 • Vipimo vya masikio
 • Lumbar puncture – Kipimo cha kuangalia bakteria kwenye maji ya uti wa mgongo
 • Cerebral angiogram – Kipimo cha kuangalia mishipa ya damu kwenye ubongo
 • Nerve conduction tests
Tiba ya ugonjwa wa kaswende
Tiba
ya ugonjwa wa kaswende inahusisha matumizi ya dawa za antibiotic za
kundi la penicillin. Dawa nyengine ni aina ya polyketides antibiotics
(doxycyline nk.) lakini hizi hazitumikia kwa wajawazito. Kwa wale ambao
wanapata madhara baada ya kutumia penicillin ni bora kumjulisha daktari
mapema. 

Tiba kwa wale wenye kaswende iliyoathiri mishipa ya fahamu ni
penicillin inayotolewa kupitia kwenye mishipa ya damu na wanahitaji
kulazwa hospitali kwa matibabu zaidi. Wale ambao wameathiriwa na
kaswende kwenye viungo vya mwili, madhara hayo sio rahisi kurekebishika
na mengine hayarekebishiki.

 
Tiba ya upasuaji
Tiba ya upasuaji kwa wale wenye madhara ya ugonjwa wa kaswende kama kwenye moyo na nk.
Wagonjwa
wa syphilitic aortitis wanaweza kutibiwa kwa angiography/angioplasty
lakini kama wana magonjwa mengine ya moyo kama coronary heart disease
basi tiba hii haifanyiki. 

 
Madhara ya ugonjwa wa kaswende


 • Magonjwa ya moyo
 • Magonjwa ya akili
 • Mtu kuwa kiziwi
 • Upofu
 • Magonjwa ya mishipa ya fahamu
 • Kupungukiwa kumbukumbu (memory loss)
 • Upungufu wa damu mwilini
 • Mimba kutoka wakati wa ujauzito
 • Kuzaa mtoto ambae ameshafariki
 • Madhara kwenye mifupa
 • Vifo vya watoto

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kaswende

 1. Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu, njia sahihi ni kuepuka kabisa ngono
 2. Wale walioathirika kuacha kufanya ngono na wenza wao hata kama wameanza tiba mpaka vidonda vipone
 3. Kwa wajawazito, kuhudhuria kliniki mapema ili kama ukigundulika kuwa na kaswende hivyo kupata tiba haraka.
 4. Epuka kugusana na majimaji yoyote yanayotoka kwa mtu aliyeathirika kwa ugonjwa huu.

Advertisement

==

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Share.

About Author

Leave A Reply