Friday, July 19

Tanzia: Askofu wa kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya, Evaristo Chengula afariki dunia

0
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya, Evarist Chengula amefariki dunia leo asubuhi akiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipokuwa anapatiwa matibabu ya moyo.

Askofu Chengula alifika jijini Dar es salaam jana, akitokea Mbeya ambako alikuwa hajazidiwa sana na alifikishwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Moyo (JKIC).

Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Padre. Charles Kitima amesema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo yaliyochangiwa na umri wake ambapo amefariki akiwa na miaka 78.

“Baba Askofu hakuwa anaumwa sana lakini alikuwa na tatizo la Moyo ambalo alikuwa analimudu kawaida na alikuwa anaendelea na kazi kama kawaida mpaka Alhamisi iliyopita ameongoza misa takatifu hali ilipobadilika ndipo alimtafta daktari wake”, amesema Padre. Kitima.

Padre Kitima amesema kuwa Askofu Chengula atazikwa jijini Mbeya siku ya Jumanne katika kanisa alilokuwa akihudumia Askofu.

Mwezi Machi mwaka huu, Askofu Chengula aliwataka wakristo kote nchini kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2019 wa Serikali za Mitaa akiwataka wananchi kumchagua mtu asiyewafanya waishi kwa kuogopaogopa.

Alitoa kauli hiyo Machi 30, 2018 alipokuwa akiongoza ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika kitaifa katika kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Fatma lililopo Mwanjelwa mjini Mbeya.

Pia katika ibada hiyo, alitolea ufafanuzi ujumbe uliotolewa na maaskofu wakatoliki akisema ujumbe ulikuwa haumlengi mtu fulani bali uliwalenga wanafiki wanaodai ni Wakristo lakini hawana imani ya Kikristo ili waweze kubadilika na kuwa watu wema.
 

Advertisement

==

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==

….

===

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Share.

About Author

Leave A Reply