Saturday, August 17

Matokeo:CCM Inaongoza Siha

0


Matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Siha  yameanza kubandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yakionyesha mgombea wa CCM, Dk Godwin Mollel akiongoza kwa mbali katika baadhi ya vituo.

Katika matokeo hayo, Dk Mollel  anafuatiwa kwa mbali  na mgombea wa Chadema,  Alvis Mossi   huku wa CUF,  Tumsifuel Mwanri  akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo.  Kituo cha Kirua–Kawate  Kata ya Siha, Wilaya ya Siha mgombea wa CCM  alipata kura  208, huku Alvis wa Chadema akipata kura 42 na Mwanri  wa CUF akipata kura  10

Katika kituo cha  Lawate namba 2 Kata ya Siha, CCM ilipata kura 300 na Chadema 21 huku CUF ikiambulia 0.

Kituo cha Lomakaa,  CCM ilipata kura 190, Chadema 10 na CUF haikupata chochote.

Pia kituo cha Ofisi ya Kijiji Sanya Juu, CCM ilipata kura 284,Chadema 54 na CUF 1.

Kwa upande wa kituo cha Sanya Juu, CCM ilipata kura 93,Chadema 50,  CUF 0, huku kituo cha Kaboko Kusini 2, CCM 403, Chadema 68 ,CUF na Sau zikiwa hazijapata kitu.

Pia Kituo kingine cha Kaboko B; CCM 106,CUF 76, Sau 0 na kituo cha Ofisi ya VEO Merali Juu1; Chadema 33, CCM 64 huku CUF na Sau vikiwa havijapata kitu. Ofisi ya VEO Merali Juu2: Chadema 22 na CCM 87.

Kituo cha Pyarita kata ya Nasai  Mgombea wa CCM alipata kura 194 huku Alvis wa Chadema akipata kura 44 na Mwanri akipata Cuf akipata kura 5.

Endelea kufuatilia matokeo zaidi hapaRead More

Share.

About Author

Comments are closed.