Thursday, August 22

Katibu wa Bunge Azungumzia Ajali ya Wabunge 6

0


Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai amesema chombo hicho cha dola kinafuatilia kwa ukaribu ajali ya wabunge sita iliyotokea jana usiku, Machi 29, 2018 mkoani Morogoro.

Kagaigai amesema baada ya kupokea taarifa hizo wamefanya mawasiliano na uongozi wa Hospitali ya Morogoro na walishauriwa kuwahamishia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Ndiyo taarifa hizo ninazo, wamepata ajali huko Morogoro, tayari tumeshafanya taratibu za kuwapeleka Muhimbili kwa huduma zaidi na ofisi yetu inawajibika kwa kila hatua,” amesema Kagaigai.

Wabunge hao ambao wote ni kutoka Zanzibar ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).Read More

Share.

About Author

Comments are closed.