Wednesday, August 21

Harmorapa Amtolea Povu Uchebe na Kudai Ameolewa na Shilole

0


Rapa wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa aliyejipatia umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake amerudi tena  na safari hii yuko na Shilole pamoja na mumewe Uchebe.

Harmorapa ameibuka na kudai kuwa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemuoa mumewe Uchebe. Huku akidai kuwa kitendo cha Uchebe kuacha kazi yake ya ufundi gereji na kumtegemea mke wake ni sawa na kuoelewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa amerusha dongo hili lililowaelekea Uchebe na Shilole:

“Uchebe mtoto wa kiume umeacha Kupiga  spana umekimbilia Kuolewa. Kwa nini badgirlshishi akuosheshe vyombo? Uchebe mtoto wa kiume rudi gereji ukapige spana la sivyo utapigwa sana vibao na shishi na kufulishwa mpaka chup*, sura yenyewe imekukunjika kama yangu utafikiri tumetoroka kwenye zui la manyani/ hiyo ndio faida ya wanaume marioo vibenteni demu wanahudumia masponsa mzigo tunakula sisi kimya kimya na chup* tunachafua sisi wahudumiaji alafu  vibenteni kama Uchebe kazi yao kutakatisha chup*”.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni, kabla hawajaoana Uchebe alikuwa fundi magari gereji lakini baada ya kufunga ndoa amekuwa akionekana kila mahali na Shilole akimsindikiza kwenye shoo zake zote hali iliyozua maneno maneno.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.