Monday, July 15

Ali Kiba Aitosa Wasafi Festival,….Asema Atakuwa na Majukumu Mengine

0
Msanii wa muziki wa Bonofleva Ali Kiba amemjibu msanii mwenzake Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’  kupitia ukurasa wake wa Instagrama kuwa amepata salamu za mwaliko wake, lakini hataweza kushiriki kwa kuwa atakuwa na majukumu mengine.,

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba ameandika; “Baada ya subra ya muda mrefu, hivi karibuni nitawatangazia bidhaa yetu pendwa ya Mofaya inapatikana wapi na kwa kiasi gani! Pamoja na shughuli rasmi ya kuizindua kitaani.

“Pia ndugu zangu #Wasafi tumepata salamu zenu, nashukuru kwa mualiko wenu, ila kwa bahati mbaya sitoweza kushiriki kwa sasa kutokana na majukumu ya kuzindua Mofaya katika nchi zingine. Hata hivyo tusingependa kuwaacha hivi hivi.

“Tupo tayari kuwapa support ya kudhamini tamasha lenu kupitia #MofayaEnergyDrinkili kuweza kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya sanaa yetu Tanzania na Africa. Management   #RockstarAfricayangu tutaendelea kuwasiliana nanyi tuweze kufanya hili jambo kubwa.”

Wasafi Festival inatarajiwa kuzinduliwa Novemba 24 mkoani Mtwara ambapo baadaye Iringa, Morogoro na mikoa mingine itafuata.

Advertisement

tang

==

Advertisement

Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==

….

===

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Share.

About Author

Leave A Reply