Sunday, August 25

BOCCO: SIMBA WANAPOINTI ZETU

0


Mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco amesema licha kushindwa kupata ushindi dhidi ya Mbeya City, ana uhakika Simba wana pointi tatu zao watakapokutana katika mchezo unaofuata wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo wa ligi kuu utachezwa Januari 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya timu hizo kukutana kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 13, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Katika mchezo huo, Azam ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Himid Mao na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya tatu sawa na Simba.

Simba na Azam zinatarajiwa kukutana kwenye mchezo huo wa ligi kuu huku ikikumbukwa katika mchezo wa awali Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Shiza Kichuya.

 Bocco alisema wanatambua ugumu uliopo katika mchezo huo kutokana na ukubwa wa timu hizo lakini watahakikisha wanapambana ili kupata ushindi na kujiongezea pointi tatu.

“Hatukuweza kupata matokeo dhidi ya Mbeya City kwa sababu hata wapinzani wetu nao walikuwa wamejiandaa, sasa tunaenda kujiandaa na mchezo unaofuata kwa kuwa tunazitaka hizo pointi tatu.

“Tunawaahidi mashabiki wetu kwamba tutaenda kupambana ili tuweze kupata pointi tatu ambazo kwetu ni muhimu sana, najua mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Simba wanaongoza ligi,” alisema Bocco.

Chanzo: salehjembeRead More

Share.

About Author

Comments are closed.