Tuesday, July 23

MADIWANI ILALA WAILALAMIKIA TARURA KUCHELEWESHA UJENZI WA BARABARA.

0


 

Na Heri Shaaban

Baraza la madiwani wa manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam,wameitupia lawama Wakala wa Barabara TARURA Manispaa ya Ilala kwa kushindwa kujenga barabara kwa wakati zilizopo ndani ya manispaa ya Ilala.

Madiwani wa Ilala walitoa malalamiko hayo katika kikao baraza la halmashauri Dar es Salaam leo wakati Diwani wa kata ya Upanga Mashariki Sultan Salim akilalamikia Wakala wa Barabara TARURA katika barabara za Mtaa wa Ismani Makao Makuu Jeshi na Urambo makao Makuu

” Sisi kama madiwani wa manispaa ya Ilala atuwaelewi TARURA utendaji wao katika barabara za wananchi wetu mfano katika eneo la makao makuu ya Jeshi utekelezaji unasua sua “alisema Sultan.

Sultan alitaka TARURA Ilala kujenga barabara kwa wakati katika miradi yote ya barabara waliosimamia .

Alisema toka serikali kuikabidhi TARURA shughuli za barabara utekelezaji wake ndani ya manispaa ya Ilala umekuwa wa kusua sua hawajengi kwa wakati.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara TARURA Mhandisi Samwel Ndoven alisema Manispaa ya Ilala wametenga shilingi bilioni 6.2 katika bajeti ya mwaka 2018 hadi 2019.

Alisema changamoto iliyokuwepo ni fedha ila wameweka utaratibu maalum katika mfumo inaelezea idadi ya barabara na gharama zake na kazi rasmi wameanza hivi karibuni .

Samwel alisema miradi itakayosimamiwa ya kuchonga barabara mbalimbali km 70 ambapo alitaja barabara zilizopo katika mpango huo kuwa ni Kitunda,Mwanagati,Kwampalange ,Tabata,Mawenzi,Kisiwani,Chanika,Msumbiji,Nzasa.

Alitaja barabara nyingine kuwa ni Kibeberu,Magore ,Kisukuru Makoka,Pugu Majohe ,Mondole,Kitunda ,Kipera,Bonyokwa ,Kisukuru,Kimanga Tasaf,Kivule ,Kinyerezi na Zimbili.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri katika baraza hilo la madiwani alipiga marufuku machinjio bubu badala yake aliwataka wananchi wa manispaa ya Ilala wale nyama ambazo zimepimwa.

Shauri alisema manispaa ya Ilala wanatarajia kuanza oparesheni hivi karibuni ya kukagua machinjio.

Naye Naibu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto aliwataka
TARURA kushirikiana na madiwani wa Ilala.

Diwani wa kata ya Ilala Saddy Kimji katika baraza hilo alipendekeza takataka ngumu zibadilishwe ziwe mali ghafi.

Share.

About Author

Leave A Reply