Sunday, August 25

Watanzania Kuneemeka kimawasiliano na Halotel

0
Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala (Kulia) pamoja na Meneja wa mahusiano wa Halotel Stella Pius kwa pamoja wakiongea na wananchi katika soko la makumbusho, Dar es Salaam, jana ,kuhusu kampeni yao mpya ya kununua bando kwa Halopesa ambapo mamilioni ya wateja kunufaika kwa kupata huduma za mawasiliano kwa bei nafuu Zaidi, ikiwa ni muendelezo wa kampeni yao ya kufikia mteja mmoja mmoja .

Katika kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano nchini, Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel imeendelea kubuni mbinu mpya kuhakikisha kwamba wateja wake wa kada zote wanapata suluhisho la changamoto ya gharama za mawasiliano na kupata huduma hii kwa urahisi zaidi.

Ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuboresha huduma, Halotel, Imepunguza gharama za mawasiliano kwa wateja wake kwa kuzindua huduma mpya ya Nunua Vifurushi maalum kwa Halopesa ili kuwawezesha wateja wa mtandao huo kuepuka gharama kubwa za mawasiliano.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo, Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Nguyen Van Son, amesema kuwa huduma hiyo itawawezesha wateja wote nchi nzima kuweza kununua vifurushi maalum kupitia Halopesa ambapo wamezingatia uhitaji wa mahitaji yao

“Huduma hii inawalenga wateja wa vipato vya chini wanaofanya mawasiliano yanayolingana na wenye vipato vya kati lakini wanapata huduma hii kwa gharama nafuu kwa kujiunga kupitia Halopesa tofauti na wateja wengine, aliongeza Son”.

Mfano; kwa mteja anayetumia shilingi mia tano (500) kwa siku, kwa sasa anaweza kujiunga na kifurushi hiki maalum kupitia Halopesa akapata hadi dakika 32 za kupiga simu mitandao yote, Mb 250 za intaneti na ujumbe mfupi (SMS) 550, vilevile kwa shilingi mia tano (500)hiyohiyo mteja anaweza kujiunga na kifushi cha wiki akapata Mb 300 za intaneti za kutumia kwa wiki nzima.

Hatuishi hapo, kwa mteja anayetumia shilingi elfu moja ( 1000) anaweza kujiunga na kupata hadi dakika 52 za kupiga mitandao yote, Mb 350 za intaneti na ujumbe mfupi (SMS) 1000 za kutumia kwa wiki nzima kujiunga kupitia Halopesa kupiga code namba *150*88# na kuchagua namba 2. ” Alisema Son.

Halopesa ni huduma ambayo inaendelea kukua zaidi, ambapo mbali na mteja kuweza kupata huduma za miamala ya kifedha, kulipia bili mbalimbali kupitia simu ya mkononi, lakini pia mteja anaweza kujiunga na vifurushi mbalimbali kwa punguzo ya asilimia 30 ya gharama kwa kiasi cha pesa atakachotumia na punguzo la kiasi hicho cha pesa atawekewa kwenye akaunti yake ya muda wa maongezi ambapo anaweza kutumia apendavyo.

Halopesa ni huduma iliyozinduliwa rasmi tarehe 15 Octoba 2015, ikiendelea kukua kwa kasi na imeenea sehemu kubwa nchini kwa asilimia 95% ya watanzania mijini na vijijini na ni ya haraka ambapo inapatikana kwa code namba ya *158*88#.

“Kwa kutumia Halopesa mteja anaweza kufanya malipo mbalimbali kama vile kutuma na kupokea fedha, kupokea au kutuma fedha kupitia benki na kulipia huduma nyingine kama Luku, Dawasco, na ving’amuzi vya televisheni mfano. DSTV, ZUKU, mifuko ya jamii wa GEPF, TCU na Polisi, kulipia michezo mbalimbali ya kubashiri kama Sportpesa na Mojabet, kununua muda wa maongezi na vifurushi mbalimbali kwa mtandao wa Halotel”, Aliongeza Son.

“Tangu tumeanza kutoa huduma kwa Watanzania tumekuwa tukizingatia sana utoaji wa huduma kulingana na mahitaji halisi na hali ya kiuchumi kwa Watanzania jinsi ilivyo, Tutaendelea kuhakikisha wateja wetu wanapata vifurushi vinavyoendana na uhalisia wa maisha yao.

Tunatarajia kifurushi hiki kitaongeza nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wetu na kwa watanzania wote, wakiwemo wafanya biashara, wakulima na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na vijijini ambako maeneo haya kwa kiasi kikubwa hutegemea njia ya simu za mkononi kuweza kuwasiliana na kupata taarifa mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia intaneti kwa uhakika.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.