Thursday, August 22

BancABC YATEKELEZA SERA YA FEDHA YA BoT

0
Mkurugenzi mtendaji wa BancABC Dana Botha akizungumza na waandishi wa habali katika ofisi zao Leo Jijini Dar es Salaam,kuhusu punguzo la tozo ya mikopo mbali mbali kwa wateja wao.

Mkurugenzi Mtendaji wa BancABC Dana Botha kulia,kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce Malai katikati wakishika bango linaloonyesha punguzo la tozo za Mikopo.

BENKI ya BancABC imesema imetekeleza Sera ya fedha ya Benki Kuu ya Tanzania(BoT) kwa kutangaza kutoa punguzo kwa wateja wake wapya kuwezesha kukopa kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji was BancABC Dana Botha amesema benki hiyo ni sehemu ya Atlasi Mara iliyosajiliwa katika soko la hisa la Londan ikiwa na lengo la kujitanua ili kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa Sahara kwa kutumia uzoefu wake na uwezo wa kukuza mitaji.

Hivyo Botha amesema watapungunza riba kwa wateja wao katika mikopo ya masharti ambayo itakuwa ni huduma ya Over draft pamoja na ya nyumba na kufafanua mwaka jana benki nyingi zilipita katika wakati mgumu wa ukwasi.

“Hivyo kufanya uwezo wa kukopesha kuwa mdogo.Kwa miezi kadhaa sasa,Serikali kupitia BoT imekuwa ikisisitiza kuhusu punguzo la riba hiyo kwa kupunguza masharti kama vile kiwango cha chini cha fedha kwa mabenki,”amesema Botha.

Ameongezea viwango vya punguzo,hati fungani za hazina na kukopesha
mabenki kwa viwango vya chini na hiyo imewezesha ukopeshaji kwa watu binafsi na kampuni mbalimbali ili kuimarisha biashara zao na hatimaye kuboresha uchumi. “Na tunajivunia kuwa kati ya benki za kwanza kutangaza wazi kuhusu punguzo hili.”

Aidha Mkuu wa kitengo cha Hazina BancABC Barton Mwasamengo amesema kuwa benki hiyo inahudumia wateja zaidi ya 60,000 ambao wanamiliki bidhaa tofauti za kibenki

Mwasomengo amesema fursa hiyo itawawezesha kuwashawishi wateja kupata mikopo ya Nyumba ambayo ilikuwa changamoto kubwa hasa kwa wananchi wa Daraja la kati na chini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha wateja binafsi na wafanyabiashara wa BancABC Joyce Mlai amemalizia kwa kusema katika kujenga nyumba wanaungana na Serikali kuwapa fursa ya kuwapatia mikopo ya Nyumba wafanyakazi wa aina zote sekta binafsi,serikalini pmoja na wafanya biashara.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.