Sunday, August 25

P SQUARE AMCHANA DIAMOND TUHUMA ZA KUCHEPUKA NA ZARI ‘MADAI YA DIAMOND NI YA KIPUUZI’

0
Mwanamuziki nyota kutoka Nigeria wa kundi la P Square, Peter Okoye amekanusha madai kuwa alishiriki ngono na aliyekuwa mke wa mwanamuziki maarufu Diamond Platinumz Diamond alimkashifu Zari Hassan kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume kadhaa wakati walikuwa katika ndoa. 

Kulingana na Diamond, Zari alikuwa alishiriki ngono na Peter punde baada ya kujifungua mwana wao wa kwanza, Tiffah Dangote. ” Zari ni mzazi mwenzangu na namuheshimu sana ila nimekuwa kimya kwa muda mrefu sana, hakuwa mwaminifu wakati tulikuwa katika ndoa, nilimnasa na wanaume kadhaa akiwemo mwanamuziki P Square,” Diamond alisema.

 Akiwa kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Cool FM, Peter alisema madai ya Diamond ni ya kipuuzi na kwamba hatazungumzia suala hilo. 

Diamond alidai hakuachwa na Zari ila yeye alikuwa tayari ashapoteza hamu ya kushiriki naye tendo la ndoa. 

Akiyajibu madai ya Diamond, Zari alidai mwanamuziki huyo ni muongo na kwamba alikuwa anataka kutafuta umaarufu zaidi kwa kumchafulia jina. 

” Iwapo utamwamini mwanaume aliyemkana mwanawe peupe kwenye redio, hivyo basi pia wewe ni mpumbavu kama yeye,” Zari alisema. 

Haya yanajiri siku chache tu baada ya Zari kudokezea kwamba amempata mchumba anayatarajia kufunga naye pingu za maisha. 

Share. Twitter Facebook Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr Email

About Author

Leave A Reply