Tuesday, August 20

WAZIRI AAGIZA STENDI YA NJOMBE KUANZA KUTUMIKA MEI 10

0


Na Amiri kilagalila-Njombe

Naibu waziri wa OR TAMISEMI mh.Joseph sinkanda kandege ameiagiza halmashaauri ya mji wa Njombe kuhakikisha kituo kipya cha mabasi kinacho jengwa mjini Njombe kuanza kutumika mapema tarehe kumi mei bila kupitisha agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Waziri ametoa agizo hilo hii leo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo huku akiridhishwa kutokana na kazi ambazo zimefanyika na kufikia hatua nzuri ya ujenzi na kuwataka mara moja kuanza kuwatangazia wananchi mara moja bila kubadilisha maagizo ya Rais.

“kwa kazi ambazo zimefanyika mimi niwapongeze lakini tarehe kumi mwezi mei stendi naomba ianze kutumika bila ya kuwa na maneno mengine yoyote ya kujitetea,na ni vizuri mkaanza kuwatangazia wenye mabasi na wenye daladala kama ambavyo mheshimiwa Rais aliwaomba wananchi wavumilie kipindi cha siku 30 hakuna namna ambavyo tunaweza kuyabadilisha maneno yale na kwa kazi ilipofikia hakuna sababu ya kuto kuanza kuitumia stendi hii”alisema Kandege

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda amesema kuwa stendi hiyo itaanza kutumika mapema baada ya kukamilika.

“stendi hii tutaikamilisha ndani ya muda tuliopewa na Rais na itaanza kutumika mala moja na sasa tumeshaanza kukutana na wadau mbali mbali kwa ajili ya kuweka utaratibu”

Naye Joseph Didas mhandisi mshauri wa mradi huo amesema wanategemea kumaliza kazi ndani ya muda ulioongezwa na mheshimiwa Rais huku kazi zilizo nje ya mkataba zikiendelea kwa mujibu wa maagizo ya waziri.

“tunategemea kwamba tumalize huu mradi ndani ya siku ambazo tumeongezewa na Rais lakini kazi ambazo ziko nje ya mkataba tutakuwa tunaendelea nazo kulingana na maagizo ya naibu waziri,kuna kazi ya kujenga barabara ya nje na nyinginezo tunaimani hizi ni ndogondogo tutazimaliza wakati stendi ikiendelea kutumika”alisema Mhandisi


Share.

About Author

Leave A Reply