Monday, August 19

WANAOANZA KAMPENI ZA UBUNGE NA UDIWANI WASHUGHULIKIWE

0


Na HERI SHAABAN
Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Ilala kimetoa agizo kwa Wana CCM wilaya Ilala ambao wameanza kampeni mapema za ubunge na udiwani washughulikiwe.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma Dar es Salaam leo, katika semina ya viongozi na Watendaji wa chama cha mapinduzi na Jumuiya zake ngazi ya Kata na matawi iliyoandaliwa na CCM wilaya .

Chuma amesema chama cha mapinduzi CCM kinaelekea katika chaguzi mbalimbali ikiwemo serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu katika chaguzi hizo kuna watu wameshaanza kutangaza nia za udiwani na serikali za mitaa kabla muda naomba wote chama kiwape adhabu.

“Naagiza pia Viongozi wa chama ambao wanawabeba Wagombea katika uchaguzi katika wilaya yangu ya Ilala wasimamishwe miezi 18 “alisema Ubaya.

Aidha alisema Wenyeviti wa Chama na Jumuiya ambao wameanza kuonyesha nia
za kugombea nafasi za ubunge au udiwani hawana nafasi labda kama wamejipima na kuona wanaweza wajiuzuru nafasi moja.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA amesema mwaka huu Manispaa Ilala imevuka lengo imekusanya kodi aslimia 73,katika robo tatu ya mwaka wa fedha 2019. tumevuka lengo amewataka wana Ilala kulipa kodi kwa wakati pesa ili serikali yetu iweze kupata fedha za kutengeneza barabara na huduma mbalimbali za jamii.

Mjema akielezea Mikopo ya Serikali alisema fedha zilizotengwa za mkopo shilingi bilioni 4,fedha zipo za kutosha na Mei mwaka huu Manispaa Ilala inatarajia kutoa mikopo ya bilioni mbili .

Aidha alisema wananchi wa wilaya ya Ilala ambao wanachukua mkopo chini ya milioni moja sio lazima kutoa hati ya nyumba.


Share.

About Author

Leave A Reply