Friday, May 24

WANANCHI MAKETE WAHIMIZWA KUTUNZA MAZINGIRA

0


Na Amiri kilagalila-Njombe

Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji pamoja na kulima kilimo mbadala ili kuepuka utoroshwaji wa moto unaotajwa kuharibu mazingira kwa kiasi kikubwa .
 
Afisa mazingira halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe Upendo Mgaya wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vijiji na vitongoji wa Kata ya Tandala wilaya ya Makete ametoa wito huo katika kikao cha  kuhimiza utunzaji wa mazingira katika maeneo yao.

“Tunaagizwa tuhakikishe tunavilinda na kuvitunza vyanzo vya maji ili tuendelee kuyapata maji ya kutosha yatusaidie katika uhai wetu”alisema Mgaya

Aidha  amewataka viongozi kutoa elimu kwa wananchi juu ya ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki maarufu kama  rambo ifikapo Juni mosi mwaka huu na kwamba baada ya Muda huo kupita sheria zitaanza kuchukuliwa kwa watakao uza kutengeneza pamoja na kutumia mifuko hiyo.
 
“Naamini mmesikia katika vyombo vya habari juu ya katazo la kutumia mifuko ya Rambo kwa hiyo tumeagizwa inapofika tarehe moja ya mwezi wa sita mwaka huu asionekane mtu anazalisha,anauza au anatumia mfuko wa Rambo kwa hiyo niombe kama viongozi kuanzia vitongoji,kijiji mpaka kata tukazidi kuhabarisha wananchi ili wapate uelewa”aliongeza Upendo

Licha ya msisitizo wa kutofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji lakini bado jamii wilayani humo inaamini nafasi ya kuruhusiwa kuendea na shughuli hata kwa mita 30 kutoka katika chanzo kutokana jiografia ya wilaya ya Makete. 


Share.

About Author

Leave A Reply