Sunday, August 25

WADAU WA MICHEZO WAHIMIZWA KUIBUA VIPAJI VIJIJINI

0


Na Frankius Cleophace Tarime

Wadau wa soka na wapenzi wa Mpira wa Miguu Wilayani Tarime Mkoani Mara wameombwa kujitokeza kwa lengo la kuanzisha Ligi mbalimbali kuanzia ngazi za Vitongoji kata hadi Wilaya ili kuibua vipajai na kuviendeleza.

Hayo yamebainishwa na mdau wa Michezo Richard Matiko wakati akikabidhi vifaa vya Michezo kwa ajili ya Ligi ngazi ya kitongoji cha Nyamisocho kijiji cha Magoma kata ya Binagi Wilani Tarime Mkoani Mara.

Justine Bhoke ni mmoja wa wachezaji katika kitongoji cha Nyamisocho amesema kuwa wamezoea kuona ligi kubwa zikifanyika katika maeneo ya Mjini na ligi nyingi zikiwa za wilaya lakini kwa kile ambacho kimefanywa na mdau wa michezo kuanzisha ligi ngazi ya Kitongoji kimewapa hamasa ya kupenda michezo.

“Huku maeneo ya Vijijini ndo kuna vijana wengi wapenzi wa soka na wanajua kweli kuchzeza mpira lakini tunashindwa kutoka kwa sababu hatuonekani pia vifaa ni changamoto pamoja na viwanja” alisema Bhoke.

Pia Matiko aliongeza kuwa endapo vijana watacheza vizuri na kuonyesha vipaji yuko tayari kuwaunga mkono hadi wanashiriki katika timu za Wilaya Mkoa hadi Taifa lengo lake nikuona vijana wanafanikiwa kimichezo.

Mdau huyo wa michezo amekabidhi vifaa vya michezo zikiwemo jezi pea Mbili, Mipira Miwili, Soksi pamoja na dawa za kutuliza Maumivu.


Share.

About Author

Leave A Reply