Saturday, August 17

VITAMBULISHO VYA JPM VYAGAWIWA KWA LAZIMA,DIWANI AJA JUU

0


Na Amiri kilagalila-Njombe

Wagongaji wa Kokoto katika jiwe la Gangalyandefu lililopo Sido Mjini Njombe wameiomba Serikali Kuwapa tafsiri sahihi juu ya nani anastahili kulipia vitambulisho vya Mjasiliamali vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na kusumbuliwa wakitakiwa kuchukua vitambulisho hivyo kwa lazima.

Wakizungumza mbele ya diwani viti maalumu (chadema) Siglada mligo Katika jiwe hilo vijana na Wazee wanaoshinda eneo hilo kujitafutia ujira mdogo wa siku wamesema kuwa wanashindwa kuelewa vyema tafsiri ya nani anastahili kulipia kwani wao ni Vibarua tu huku Wengine wakiwa ni wamiliki wa Eneo hilo kwa leseni Maalumu kutoka Ofisi ya Madini lakini Wamekuwa wakilazimishwa kulipia Vitambulisho hivyo.

“Hili swala la vitambulisho kweli ni shida kwetu na kuna baadhi ya watendaji wamekuja hapa wakasisitiza mwisho tarehe 15 mwezi wa tano na asiye kuwa navyo basi hataruhusiwa kufanya kazi katika eneo hili,lakini pia tuliambiwa tutaletewa na tenga kuja kutuzoa hapa hakika tulitishika mno istoshe kuna wakina mama hapa wanajitafutia mia mbili kwa siku kwa kuwa ni vibarua na mda mwingine hazitoki kwa wakati wanataka twende wapi”walisema baadhi ya wagongaji wa kokoto

Diwani wa Viti Maalumu Kata ya Njombe Mjini Siglada Mligo amezungumza na Wagongaji hao wa kokoto katika eneo hilo ambapo amesema kuwa kwa mujibu Wa Maagizo ya Rais Vitambulisho hivyo vinawahusu Wajasiriamali ambao wanafanya Biashara na Si Vibarua kama ambavyo wamekuwa wakilazimishwa kulipia.

“mpango wa kugawa vitambulisho kwa wajasiriamali wenye sifa ambao walikuwa wakisumbuliwa na halmashauri ushuru wa shilingi mia mbili ubaki vile vile ila mpango wa kugawa vitambulisho ili viishe hii sio sawa,mimi nitoe wito kwa watendaji ambao wamevipokea vitambulisho kwa maagizo vitambulisho hivyo viishe hatutaelewana nao sisi tunataka vitambulisho viuzwe kwa mtu mwenye sifa na sio vigawiwe lengo viishe”alisema Siglada Mligo

Akifafanua suala hilo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema kuwa mtu ambaye anatakiwa kuwa na kitambulisho hicho ni yule ambaye Mapato yake hayazidi Milioni nne kwa Mwaka na kuahidi kwenda kutembelea eneo hilo ili kujua kiini hasa cha Mgogolo huo.

“Mimi maelekezo niliyo nayo ni yoyote ambaye anafanya biashara na mapato yake ghafi hayazidi milioni nne kwa mwaka ndiye anayetakiwa kuwa na kitambulisho hicho sasa hao wanaosema wanalazimishwa wenyewe mapato yao ni shilingi ngapi?kwa hiyo hakuna tatizo nitakwenda hapo ili nikajiridhishe ndio niwe na neno la kusema”alisema Ruth msafiri


Share.

About Author

Leave A Reply