Wednesday, August 21

TARURA NJOMBE KUTATUA CHANGAMOTO ZA BARABARA

0


Na Amiri kilagalila-Njombe

Wakala wa barabara (TARURA) mijini na vijijini mkoa wa Njombe umekiri kuwepo kwa changamoto ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na kuahidi kuzifanyia kazi kutokana madhumuni ya serikali.

Mhandisi Ibrahim Kibasa ni Mratibu wa TARURA mkoa wa Njombe akizungumza na mtandao huu mara baada ya kufikiwa na malalamiko ya Wananchi wa kijiji cha kitandililo halmashauri ya mji wa makambako,amesema kuwa changamoto hiyo ipo hivyo Tarula wanaendelea na kuifanyia kazi.

“ni kweli hiyo changamoto ipo na kama wataalamu pia tunatakiwa kuifanyia kazi kwasababu madhumuni ya serikali inavyoleta fedha ni kuhakikisha tunafanya ukarabati wa barabara kama inavyostahili kwa kukidhi ghara ya fedha iliyoletwa,muda uliopangwa kutekeleza kimkataba lakini pia na ubora unaotakiwa, kwa hiyo sisi kama Tarula kwa kweli tumejipanga vizuri na tunaenda vema”alisema Kibasa

Awali Wananchi wa kijiji cha kitandililo halmashauri ya mji wa huo,wakati wakizungumza na diwani wa kata hiyo IMAN FUTE kwenye mkutano wa hadhara, walisema kuwa kutokana na barabara hizo kulimwa chini ya kiwango na bila kuwekewa makaravati imepelekea miundombinu hiyo kuharibika kwa muda mfupi.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa kutokana na hali ya kijiji chao kutegemea zaidi katika shughuli za kilimo wameshindwa kusafirisha mazao yao kutokana na uwepo wa miundombinu isiyo pitika.

Akizungumzia changamoto hiyo diwani wa kata IMANI FUTE amewataka wananchi kuacha kupitisha mifugo hususani ng’ombe barabarani kwa kuwa inachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu miundombinu.

“kutembeza mifugo mfano Ng’ombe kwenye barabara ni kosa kisheria kwa hiyo niwaombe tuache kutembeza mifugo kwenye bara bara na kwa maana hiyo tutengeneze miundombinu pembezoni mwa barabara ambapo mifugo yetu itapita kwasababu mifugo tunaihitaji na ili kuvuka barabara tafsiri yake ni lazima tuwe na kieneo kwa hiyo hili afisa mifugo hili niwakabidhi wenzangu”alisema Fute


Share.

About Author

Leave A Reply