Thursday, August 22

SIMBA HII SASA SIFA NA LEO TENA, YAICHAPA BIASHARA UNITED 2-0

0


Na Shabani Rapwi

Simba SC imeendeleza wimbi la ushindi hii leo kwa kuichapa Biashara United 2-0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Karume, Musoma.

Magoli yote mawili ya Simba yamewekwa kambani na Nahodha John Bocco dakika ya 34 kwa shoti kali lililomshinda mlinda mlango na dakika ya 41 akimalizia pasi ya Asante Kwasi.

Ushindi huo unawafanya mabingwa hao watetezi kufikisha alama 69 nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu, nafasi ya tatu Azam FC wakiwa na alama 66 huku Yanga wakisalia kileleni na alama 74.

Baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo huo unamfanya John Bocco kufikisha magoli 14 huku Meddy Kagere na Salim Aiyee wakiwa na magoli 16.

Pia katika mchezo huo mchezaji wa klabu ya Simba, Haruna Niyonzima alitolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 71 baada ya kucheza mchezo usio kuwa wa kiungwana.


Share.

About Author

Leave A Reply