Wednesday, August 21

SERIKALI IMETOA ZAIDI YA BILIONI 40 KUTEKELEZA MIRADI YA UMEME VIJIJINI

0


Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 40 ili kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Samunge alipokwenda kukagua kazi ya kuunganisha umeme katika Kata hiyo, Dkt. Kalemani alisema Vijiji vyote vya kata ya Samunge vitapata umeme.

“ Vijiji vyote haviwezi kuwekewa umeme kwa siku moja, lakini ni hakika vyote vitawekewa umeme, endeleeni kulipia ili kiunganishwa na huduma ya umeme“, alisisitiza Dkt. Kalemani.

Aidha, alimtaka Mkandarasi Kampuni ya Nipo Group, kukamilisha kazi ya kuunganisha umeme katika vijiji na vitongoji vyote vya Kata ya Samunge na Digodigo ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande wake Mzee Ambikile Mwasapila maarufu kwa jina la mzee wa kikombe, ambaye nyumba yake imewashwa umeme,
ameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Nishati kwa kufikisha huduma hiyo muhimu kijijini hapo na kuwahamasisha wanakijiji wengine kulipia ili wawekewe umeme.

Katika ziara yake ya siku mbili Mkoani Arusha, Dkt. Kalemani pia aliwasha umeme Kituo cha Afya cha Digodigo, Shule ya Msingi Bisikene na Ofisi ya Afisa Tarafa Digodigo.


Share.

About Author

Leave A Reply