Thursday, August 22

RC MAKONDA AFAGILIA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA ILALA

0


NA HERI SHAABAN

MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Paul Makonda ameipongeza wilaya ya Ilala kwa kusimamia ujenzi wa miradi ya Serikali inayofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Makonda aliyasema Dar es Salaam leo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Ilala kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika serikali ya awamu ya tano zikiwemo barabara zilizofadhiliwa na Wold Bank Mtaa Mbaruku Kata ya Gerezani Kiwalani ambayo imekamilika kwa asilimia 90 na Gongolamboto Kampala nayo lami asilimia 90.

“Nawapongeza Mkuu wa Wilaya Wilaya ya Ilala Sophia Mjema na Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Shauri kusimamia vizuri miradi mkakati ya barabara ili iweze kutumika na wananchi.

Makonda aliyasema miradi hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM na miradi yote ameagiza imalizike kwa wakati.

Aidha Makonda alimwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kusimamia ujenzi wa hospitali ya Wilaya eneo la Kivule mpaka kufikia Juni 30 iwe imemalizika wananchi waweze kupata huduma.

Alisema Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli ni sikivu inazogeza huduma za maendeleo karibu na wananchi ili waweze kupata huduma za jamii sio wananchi kufuata huduma.

Alisema miradi ya mkakati ya serikali katika Mkoa huo imegharimu zaidi ya Tilion 3 ametaka ajira zote wapewe wazawa na vifaa vya matilio zinunuliwe katika viwanda vya ndani ili kodi ziongezeke.

Kwa upande mwingine Makonda amemwagiza Ofisa wa TARURA kuweka utaratibu wa kujenga daraja la muda eneo la Stakishari Segerea.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Wilaya Sophia Mjema alisema ujenzi wa soko la Kisasa eneo la Kisutu litakamilika baada ya miezi 18 mara baada kuisha wafanyabiashara watarudi katika eneo lao.

Mjema alisema miradi yote hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi CCM na itakwisha kabla ya uchaguzi mkuu 2020

Akielezea kituo cha afya Buguruni Plan Mjema alisema jengo hilo imekamilika kwa asilimia 90 jengo la kisasa na vifaa vya matibabu vyote vipo.


Share.

About Author

Leave A Reply