Monday, August 26

RC AAGIZA WATENDAJI WASIOTIMIZA LENGO LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA JPM KUJIELEZA KWA BARUA

0


MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amesema kuwa ifikapo June saba mwaka huu wataendesha tathimini ya zoezi la uuzwaji wa vitambulisho vya wajasiriamli na watendaji ambao watakuwa hawajafanya vizuri watasimamishwa kazi.

Dkt.Mahenge ameyasema hayo wilayani Chemba alipokuwa akihitimisha ziara yake aliyozunguka katika wilaya zote kukagua,kugawa na kuhamasisha wajasiriamali kuwa na vitambulisho hivyo.

Akiwa wilayani humo,Dkt Mahenge amepokea taarifa ya uendeshaji wa zoezi hilo ambalo imeonyesha kuwa baadhi ya watendaji hawajafikisha nusu ya mauzo ya vitambulisho hivyo ambapo amewataka kuongeza kasi kwani baada ya tahimini watendaji watakao kuwa hawajafanya vizuri wataondolewa kazini.

“Kama hakuna matokeo tunafanya tathimini tarehe saba mwezi ujao,tutawasimamisha kazi wale ambao watakuwa hawajafanya vizuri,watu watilie maanani zoezi hili”Alisistiza.

Aidha pia amemuagiza katibu Tawala msaidizi ngazi ya Mkoa Aziza Mumba kumuandikia barua ya kujieleza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Semistatus Mashimba kuwa ni kwa nini hajafanya vizuri lakini pia naye Mkurugenzi huyo kuwaandikia barua za kujieleza watendaji wote ambao hawajafikia nusu ya uuzaji wa vitambulisho hivyo,

Kwa upande wake Mkurugenzi  Mashimba amekiri kuyapokea maelekezo hayo na kusema kuwa tayari alikwisha chukua hatua kwa baadhi ya watendaji ambao hawakufikia lengo la zoezi hilo huku Mkuu wa Wilaya hiyo Saimon Odunga akiahidi kuendelea kusimamia suala hilo kwa nguvu zake zote na kuhakikisha kuwa kila mjasiriamali anakuwa na kitambulisho.


Share.

About Author

Leave A Reply