Sunday, August 25

RAIS MAGUFULI AWAAGIZA MAWAZIRI TANZANIA KUITISHA KIKAO CHA KAMATI YA PAMOJA YA TANZANIA NA NAMIBIA

0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza Mawaziri wa Tanzania kuitisha kikao cha Kamati ya Pamoja ya Tanzania na Namibia (Joint Permanent Commission – JPC) ndani ya kipindi cha miezi 2 ili kujadiliana juu ya fursa mbalimbali za ushirikiano wenye manufaa kwa nchi hizo.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo tarehe 27 Mei, 2019 wakati wa mazungumzo rasmi kati yake na Rais wa Jamhuri ya Namibia, Mhe. Dkt. Hage Geingob yaliyofanyika katika Ikulu ya Windhoek nchini Namibia ambako ameanza Ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku 2 nchini humo.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maagizo hayo baada ya yeye na Mhe. Rais Geingob kupokea taarifa kuwa kikao cha JPC hakijafanyika tangu mwaka 1999 na kusababisha masuala mengi yakiwemo ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kutopata msukumo wa kutosha.

Amebainisha kuwa licha ya uhusiano wa kihistoria na kidugu wa Tanzania na Namibia ulioasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Namibia Mhe. Sam Nujoma, nchi hizo zimekuwa na kiwango cha chini cha ushirikiano wa kibiashara baina yake ambapo katika mwaka uliopita biashara iliyofanyika ilikuwa na thamani ya shilingi Bilioni 59.556 tu na kwamba nchini Tanzania kuna kampuni 2 tu za Namibia zinazofanya biashara.

Pamoja na kutoa maagizo hayo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Rais Geingob kwa kumualika kufanya Ziara Rasmi ya Kitaifa nchini Namibia na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wowote unaohitajika ikiwemo kushirikiana katika masuala ya kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii, usafiri wa anga, biashara, uwekezaji, utamaduni na kufundisha lugha ya Kiswahili ambacho baadhi ya nchi za Afrika zimeridhia kianze kufundishwa katika shule zake.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amesema kwa kutambua uhusiano wa kihistoria na kidugu, Tanzania inakamilisha maandalizi ya kufungua Ubalozi wake Jijini Windhoek ili kurahisisha masuala mbalimbali ya uhusiano, hususani katika uchumi ambayo yapo nyuma.

Kwa upande wake Mhe. Rais Geingob amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kufanya ziara hiyo na amesema Namibia inatambua na kuenzi mchango mkubwa wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerere na Watanzania katika juhudi za ukombozi

Share.

About Author

Leave A Reply