Monday, August 26

MWILI WA BABA YAKE RAIS WA DRC, TSHISEKEDI KUREJESHWA NYUMBANI

0


Kinshasa, DRC.

Familia ya aliyekuwa kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Étienne Tshisekedi wa Mulumba, imesema mwili wa kiongozi huyo, utarejeshwa nyumbani tarehe 30 mwezi huu wa mei, na kuzikwa tarehe 01 juni.

Miaka miwili imepita tangu Étienne Tshisekedi, ambaye ni baba wa rais wa sasa Felix Tshisekedi, alipofariki dunia akiwa mjini Brussels nchini Ubelgiji mwezi Februari mwaka 2017.

Baada ya kifo chake kulizuka utata ni wapi atazikwa. Uongozi wa chama chake cha UDPS, ulitaka azikwe kwenye makao makuu ya chama hicho, katikati ya jiji kuu Kinsasha, lakini serikali wakati huo ikiongozwa na Rais Joseph Kabila ikakataa.

Hadi kufariki kwake, alikuwa kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, akiongoza chama cha UDPS, lakini pia aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu wakati wa utawala wa rais wa zamani Mobutu Seseko mwaka 1991,1992-1993 na baadaye 1997.

Mzee Tshisekedi aliwahi kuwania urais mara kadhaa nchini humo dhidi ya rais wa zamani Joseph Kabila.


Share.

About Author

Leave A Reply