Sunday, August 18

MTOTO WA MWAKA MMOJA AFUNGIWA NDANI USIKU,MAMA AENDA KLABU KUTAFUTA PESA

0


Na Amiri kilagalila-Njombe

 Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 5 (jina linahifadhiwa) ameachwa na mama yake ndani usiku, na mama huyo kwenda kujiuza Kwenye klabu za usiku maarufu kama (Night Club) kwa madai ya kutafuta fedha za kumtunza mtoto huyo.
 
Tukio hilo limefanywa na mama huyo aliyejulikana kwa jina la Diana Joel Kyando (22) usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Dombwela katika mji mdogo wa Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe ambapo majirani ndio waliomtoa mtoto huyo ndani baada ya kumsikia akilia kwa muda mrefu usiku
 
Akizungumza kwenye ofisi za Afisa Mtendaji kata ya Iwawa wakati akihojiwa na Afisa mtendaji wa Kata hiyo Devota Paul, mama huyo amesema ugumu wa maisha na kukosa fedha za matunzo kutoka kwa baba wa mtoto ndicho kimemfanya kufikia uamuzi huo wa kwenda kujiuza ili apate fedha
 
“Yote haya yamenikuta kwasababu ya ndugu zangu baba ake alitaka kuzaa lakini wanaogopa ndugu zangu,nilienda serikalini wazazi wa baba mtoto wenyewe waliahidi kutoa hela za matunzo ya mtoto lakini walisema wanawaogopa ndugu zangu kwa kuwa wanasema walifukuzwa kama mbwa walipokuja nyumbani”alisema mama wa mtoto
 
Jirani Bibi Alatwegha Sanga aliyemsikia mtoto huyo akilia kwa muda mrefu ameelezea namna tukio hilo lilivyotokea na alivyoshirikiana na majirani kumnusuru mtoto huyo
 
“Nilisikia mtoto analia huko ndani kwa mda mrefu nikaangali nikamwita mtoto wangu twende tukaangalie tukakuta mlango umefungwa na kufuli kabisa tukiata majirani nikasema tuokoe mtoto, ndio tukajitahidi kufungua mlango tukamuokoa mtoto”alisema Alatwega sanga
 
Afisa mtendaji wa Kata ya Iwawa Devota Paul amesikitishwa na kitendo hicho na kuitaka jamii kufichua vitendo kama hivyo ili hatua zichukuliwe kwa kuwa vitendo kama hivyo vimekuwa vikitokea lakini vinafumbiwa macho na wanajamii wenyewe
  
Kwa upande wa jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia wametoa kauli kuhusiana na tukio hilo
 
“Ninaitwa afande Edward nafanya kazi katika kitengo cha dawati la jinsia na watoto nipo Makete,mimi nataka niseme kuwa hii hali ipo sana, na ni tatizo sugu kwasababu kesi nilizonazo ofisini kuhusu watoto ni nyingi ila kwa muamko huu inaonyesha elimu imeanza vizuri kuonekana kwenye jamii,sasa nikianza na huyu nadhani itakuwa ni funzo kwa wengine”Alisema Edward


Share.

About Author

Leave A Reply