Saturday, August 24

MRADI WA BACKBONE WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100, VIJIJI 121 VYAUNGANISHWA NA HUDUMA YA UMEME

0


Leo tarehe 24/5/2019, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika Kijiji cha Chibwegere wilayani Mpwapwa katika Jimbo la Kibakwe.

Kijiji hicho kimepata umeme kupitia mradi wa Backbone ( kV 400) unaotoka Iringa hadi Shinyanga. Hii imefanya Serikali kutekeleza lengo la kupeleka umeme kwenye Vijiji 121 vilivyopangwa kusambaziwa umeme kupitia mradi huo.

Kwa Mkoa wa Dodoma vijiji 39 vilipangwa kupelekewa umeme kupitia mradi huo na vyote vimeshawashiwa umeme na mkandarasi OK Electrical Contractors & Services.

Kutokana na mradi huo kutakiwa kukamilika Mei 30, 2019, Naibu Waziri ameiagiza TANESCO kuanzisha operesheni UNGANISHA UMEME kwa wananchi wanaopitiwa na mradi huo na kuhamasisha matumizi ya UMETA.


Share.

About Author

Leave A Reply