Saturday, August 17

MBUNGE AUNGA MKONO KAMPENI YA MAMA SAMIA,AKABIDHI VITANDA VYA KUJIFUNGULIA

0


Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula ameunga mkono harakati ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan inayolenga uzazi salama na kupunguza vifo vya wajawazito yenye kauli mbiu “Tuwavushe Salama, Maneno sasa basi ni vitendo”, kwa kutoa msaada wa vitanda vinne vya kujifungulia wajawazito katika Zahanati ya Mhandu vyenye thamani ya sh. 11,200,000.00.

Mhe. Mabula amekabidhi msaada huo Leo kwa uongozi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuwezesha Zahanati ya Mhandu kuanza kazi Mara moja kutokana na agizo la mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongella aliyetembelea Zahanati hiyo juzi.

Zoezi la makabidhiano limefanyika katika Zahanati ya Mhandu na kuhudhuriwa na kaimu Mkurugenzi wa halmshauri ya Jiji la Mwanza ambaye ni Mganga Mkuu wa Jiji Dkt. Juma Rajabu Mfanga, Diwani Kata ya Mhandu Mhe. Constantine Sima, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Ahmed Misanga, Katibu Mbunge Jimbo la Nyamagana Bi. Florah Magabe na Bi. Susan pamoja na Mtendaji wa Kata, wenyeviti wa Mtaa, viongozi wa CCM Kata.


Share.

About Author

Leave A Reply