Friday, August 23

KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA ILALA WAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

0


NA HERI SHAABAN
Kamati ya fedha Manispaa Ilala imeanza ziara endelevu kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Manispaa ya Ilala.

Ziara hiyo endelevu imeanza Dar es Salaam leo ikiongozwa na Kaimu Meya wa Manispaa hiyo Omary Kumbilamoto,akizungumza katika ziara hiyo Kumbilamoto alisema ziara hiyo ni kila baada ya robo ya mwaka.

Kumbilamoto amesema katika ziara hiyo wanakagua miradi mbalimbali ikiwemo miradi mkakati dhumuni kujilizisha fedha ya Serikali iliyotolewa na kujua mradi jinsi unavyoendelea.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya fedha ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mzinga Job Izack aliagizaTARURA watoe taarifa za kazi katika miradi ya barabara manispaa ya Ilala.

Izack alitoa tamko hilo kuwataka TARURA kufatilia miradi ya barabara za Manispaa ya Ilala kufuatia kushindwa kusimamia miradi yao inavyotakiwa.

“Kamati ya fedha Manispaa ya Ilala leo imekagua miradi ya barabara zake ambazo zipo halmashauri ya Ilala katika ukaguzi huo tumekumbana na changamoto katika barabara ya Kimanga zaidi ya miaka minne bado kuisha tulipofatilia mara ya mwisho Tarura wamefika JANUARY mwaka huu kukagua barabara ya Kimanga huku wananchi wakitoa lawama kuhusiana na ujenzi huo kukwama alisema Izack.

Aliwataka TARURA Wilaya ya Ilala kufatilia miradi yao ya barabara na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi jinsi inavyoendelea miradi hiyo unatumia fedha nyingi za serikali.

Aidha pia aliagiza kila Mkuu wa Idara awepo katika ziara marufuku kutuma mtu au Msaidizi wa mradi wengi wasaidizi uwezo wao mdogo .


Share.

About Author

Leave A Reply