Wednesday, August 21

KAMANDA WA POLISI MKOA WA IRINGA ATHIBITISHA KUTOKEA AJALI MLIMA KITONGA

0


Watu kadhaa wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea katika eneo la mlima Kitonga iliyohusisha basi la kampuni ya Sweet Afrika ya Njombe-Dar es Salaam. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwa kueleza kuwa chanzo ni dereva ameshindwa kulithibiti basi. 

“Limepata ajali eneo la Kitonga baada ya kugonga gema, katika ajali hii kuna majeruhia kadhaa ambao hawajafahamika lakini hakuna vifo,” amesema. 

Ameendelea kwa kusema, “Chanzo cha ajali ni mwendo wa dereva ameshindwa kulimudu gari hilo wakati likiteremka mteremko wa Kitonga,”


Share.

About Author

Leave A Reply