Sunday, August 25

JUMUIYA YA WAZAZI ILALA KUTOA ELIMU YA MAADILI

0


Na Heri Shaaban

JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Ilala imesema ina mkakati endelevu wa kutoa elimu ya maadili kwa vijana kufuatia vijana wengi kumomonyoka kwa maadili.

Mkakati huo wa kutoa Elimu ya maadili kwa Vijana mbalimbali Wilayani Ilala utaongozwa na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala,Jumuiya ambayo jukumu lake la kwanza kuangalia malezi ya vijana.

“Akizungumza katika Kongamano la Maadili Kata ya Liwiti Wilayani Ilala, Katibu wa Elimu na Malezi na Mazingira Jumuiya ya Wazazi Wilaya hiyo Wilson Tobola alisema mpango huo wa kutoa Elimu ya maadili ni endelevu kila kata

Tobola alisema katika wilaya ya Ilala kuna majimbo matatu elimu hiyo ya maadili itafanyika kwa lengo la kuwapa elimu hiyo wazazi wakazungumze na watoto wao.

“Watoto wanapokuwa na maadili mazuri sifa zote zinakwenda kwa wazazi kwa kuwalea vizuri watoto wao ili Taifa liwe vijana wa nguvu kazi imara “alisema Tobola.

Aidha Tobola alisema suala la maadili linagusa sehemu nyingi alitaka ngazi ya familia kwanza kumtanguliza Mwenyezi Mungu kwa kila jambo na jumuiya hiyo itashirikiana na Wazazi elimu ya maadili itolewe kuanzia ngazi ya kata hadi mtaa kila jumuiya lazima wafanye Kongamano la maadili.

Alitumia nafasi hiyo kupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kwa kusimamia miradi mikubwa na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi .

Alisema Watanzania lazima tuwe Wazalendo katika kukemea mabaya watoto walelewe katika mazingira bora.

Kwa upande wake Mgeni rasmi Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC DSM) Yusuph Nasoro alisema Vijana ni Taifa la kesho Wazazi ndio wenye jukumu la malezi ya vijana ili Taifa liweze kusonga mbele lazima Vijana wawe na maadili mema.

Nasoro alisema Wazazi ndio wenye zamana ya kulea watoto katika malezi bora ili wawe nguvu kazi ya Taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Lucas Rutainurwa alisema katika wilaya ya Ilala mwaka 2018 wameandikisha wanafunzi wa shule za msingi wengi na kiwango cha ufaulu mwaka 2018 kimeongezeka matarajio mwaka huu wanafunzi watafaulu zaidi .

Lucas alielezea uchaguzi wa Serikali za Mtaa alisema wamejipanga vizuri kwa kuchukua dola mitaa yote watashinda kwa kishindo.

Aliagiza kila kikao cha jumuiya hiyo lazima ajenda za maadili ziwepo na kujadiliwa na kufanyiwa kazi.

Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God
TAG Amani Christian Centre
DKt. Lawwrence Kametta akielezea maadili alitaka wanaume wabaki kuwa Wanaume na Wanawake wabaki kuwa wanawake .

Mchungaji Kametta pia alielezea suala la ushoga aliwataka wazazi wabebe jukumu la kuwakataza watoto wao wasipende jinsia nyingine kama ni mwanamke abaki kuwa mwanamke na kama mwanaume abaki kuwa mwanaume.

Mwisho

Share.

About Author

Leave A Reply