Sunday, August 18

JE, UNAJUA JINSI AMBAVYO MAJINA YA VIMBUNGA MBALIMBALI HUPATIKANA? KARIBU UFUATILIE HAPA

0


Na Japhet Matarra.

JE, umewahi kusikia vimbunga mbalimbali vikiwa na majina ya kushangaza, kuna kilichoitwa Idai kilichosababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe mwezi uliopita Machi katika kile ambacho Umoja wa mataifa ulisema ni janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kushuhudiwa kusini mwa Afrika.

Kuna kimbunga Matthew ambacho kiliyakumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na baadhi ya majimbo ya Marekani mwezi Oktoba mwaka 2016. Achilia hivyo, mwezi uliopita kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa huko jimbo la Florida Marekani.

Lakini mpaka sasa kimbunga kinachokumbukwa sana ni kile kinachojulikana kwa jina la Katrina, ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi na Alabama huko huko nchini Marekani.

Je, vimbunga hivi hupewa vipi majina?

Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina na Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina makao yake makuu nchini Uswizi.

Zamani, ni majina ya kike pekee yaliyotumiwa lakini kuanzia 1979, majina ya kiume yalianza kutumiwa. Huwa kuna makundi sita ya majina ambayo hutumiwa kwa mzunguko. Hii ina maana kwamba majina yaliyotumiwa kwenye vimbunga mwaka hu hayatatumiwa tena hadi 2022.

Majina kwenye orodha hii yanaweza kubadilishwa na WMO.

Orodha hii ilianza kutumiwa mwaka 1979. Kabla ya hapo, jina la kimbunga Fern lilibadilishwa mwaka 1966 na badala yake kukatumiwa Frieda. Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu kubadilishwa kwake.

Majina yanavyoacha kutumiwa

Baadhi ya majina huacha kutumiwa, hasa kunapotokea uharibifu mkubwa sana au hasara kubwa, kiasi kwamba kutumia tena jina hilo kutafufua kumbukumbu zenye uchungu.

Mfano ni kimbunga Katrina kilichoua watu 2,000 mwaka 2005 na kusababisha uharibifu mkubwa Marekani. Kimbunga hicho kiliwaacha watu milioni moja bila makao. Mji wa New Orleans, Louisiana uliathirika sana.

Katika WMO kuna kundi la wataalamu liitwalo Kamati ya Vimbunga vya Tropiki ambalo hukutana kila mwaka. Kundi hilo ndilo huamua ni majina yapi yatatumika tena na ni yapi yataacha kutumiwa.

Majina yaliyoachwa kutumiwa
tofauti na hili la Katrina, yapo mengine ambayo yameacha kutumiwa. Mfano jina la Mitch, lililotokana na kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 huko Honduras na Nicaragua, hivyo halitumiwi tena, na hicho ndicho kimbunga kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Kimbunga kingine ni cha Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011, ambavyo pia vilisababisha uharibifu mkubwa na majina hayo hayatumiwi tena.

Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000 maeneo ya Martinique, Barbados na St Eustatius. Wakati huo majina hayakuwa yameanza kutumiwa kurejelea vimbunga.

Majina yaliyoachwa kutumiwa tangu 1954.

Katika maeneo mengine duniani, huwa kuna utaratibu tofauti wa kuvipa majina vimbunga. Lakini majina yote hupitia kwa WMO. Kwa mfano, maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini, kuna jedwali la majina ambalo kila taifa linaloathirika huchangia.

Baada ya kimbunga kutokea, kimbunga kinachofuata hupewa jina linalofuata. Kwa mfano, kimbunga cha kwanza huitwa Damrey (kimbunga cha kwanza Cambondia) na kitakachofuata hufaa kuitwa Kaikui (jina la kwanza China).

Kimbunga cha sasa maeneo hayo ni Chaba (jina la nafasi ya nne Thailand). Kilichotokea majuzi kiliitwa Megi na ambacho kiliathiri maeneo ya China na Taiwan. Jina hilo ni la nafasi ya nne chini ya majina ya Korea Kusini.

Aidha, ni vyema tufahamu kuwa majina ya vimbunga na tufani yalianza kutumiwa Uingereza na Ireland, kwa majaribio, na kuna jina kwa kila alfabeti, isipokuwa Q, U, X, Y na Z, ambazo ndio utaratibu unaotumiwa kuvipa majina vimbunga Atlantiki Kaskazini.

Share.

About Author

Leave A Reply