Saturday, August 24

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUENDESHA KAMBI KWA AJILI YA UPASUAJI WA MATUNDU MADOGO 

0


Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) itaendesha kambi kwa ajili ya upasuaji wa matundu madogo (Endoscopic Surgery) kuanzia tarehe 7 mpaka 21 mwezi Juni, 2019.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Januarius Hinju, anasema kambi hiyo ya wiki mbili itaendeshwa kwa ushiriano kati ya madaktari bingwa wa BMH na wenzao kutoka Marekani.

“Tunawakaribisha watanzania na hasa wakazi wa Dodoma na mikoa ya jirani wenye matatizo ya uzazi, kutokushika mimba, ngiri (hernia) waje BMH kuanzia sasa kwa ajili ya uchunguzi ili watakaokutwa na matatizo wapangiwe huduma hiyo ya upasuaji wakati wa kambi hiyo,” anasema Dkt Hinju, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa BMH.

Dkt. Hinju anasema upasuaji wa matundu madogo ni upasuaji wa kisasa ambao una faida kubwa kwa mgonjwa kulinganisha na upasuaji wa kawaida.

Alitaja baadhi ya faida hizo kuwa ni pamoja na muda mchache anaotumia mgonjwa kupona baada ya upasuaji, maumivu kidogo pamoja na mgonjwa kutokutokwa na damu nyingi wakati wa upasuaji.

BMH inaendesha kambi hii yenye lengo la kuimarisha huduma za kibingwa kwa mwaka wa pili mfululizo katika Hospitali hiyo. Kambi ya kwanza ilifanyika Julai mwaka jana.

Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano

Hospitali ya Benjamin Mkapa


Share.

About Author

Leave A Reply