Sunday, August 25

HALMASHAURI ZAOMBWA KUJIFUNZA NJOMBE UJENZI WA SOKO

0


Na Amiri kilagalila-Njombe

Halmashauri zingine Nchini zimeombwa kujifunza namna ujenzi wa mradi wa soko kuu la Njombe unavyojengwa ili kuendana na ujenzi wa majengo yenye viwango.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Tamisemi mh.Joseph sinkanda kandege wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa soko kuu la Njombe Mjini.

“Miongono mwa masoko ambayo yanajengwa kwa ustadi mkubwa ni pamoja na hili soko la Njombe TC kwanza nawapongeza kwa kuchagua mradi huu na uhakika mradi ukikamilika kwa kiwango wanachotarajia itakuwa ni miongoni mwa Miradi mizuri kabisa,halmashauri Zingine waje kujifunza katika mradi huu”

Waziri ameongeza kuwa

“Ramani hii nimeridhika nayo ni ramani ya kisasa soko likikamilika litakuwa ni miongoni mwa masoko ya kisasa katika halmashauri zetu,nampongeza mkurugenzi na timu yake,wilaya na mkoa na sisi kama serikali miradi kama hii tutatoa sapoti ili ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kunufaika nayo”alisema Kandege

Soko hilo linaloghalimu zaidi ya bilioni saba linategemewa kukamilika mwezi wa sita na kuanza kuwanufaisha zaidi ya wafanyabiashara 1000 mjini Njombe.


Share.

About Author

Leave A Reply