Saturday, August 24

DC MAKETE AAGIZA MWENYEKITI WA KIJIJI AKAMATWE

0


Na Amiri kilagalila-Njombe
 
Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Mh Veronica Kessy amemuagiza Afisa mtendaji wa Kata ya Kipagalo kushughulikia haraka madai ya wanawake wawili wa kata hiyo wanaodai kudhulumiwa malipo yao ya kusomba mchanga wakati wa ujenzi wa ghala la Matunda katika kijiji cha Madihani
 
Mkuu wa wilaya ametoa agizo La kukamatwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Madihani Abinel Mbilinyi na mwananchi aliyetambulika kwa jina moja la Thomasi baada ya kuruhusu wananchi kutoa maoni yao kuhusu ghala hilo kabla halijakabidhiwa rasmi kwa serikali, ambapo mwanamama Jenifa Mbwilo amejitokeza na kudai kuwa hajalipwa na mkandarasi shilingi 150,000/- yeye pamoja na mwenzake kutokana na kufanya kazi ya kusomba mchanga.

 “Mtendaji wa kata hawa wa mama wapate haki yao,kamata mwenyekiti wa kijiji,Thomas watoe hiyo fedha hawa wamama wapate haki yao na unipe ripoti,jumatatu ijao nipewe mrejesho kwamba wamelipwa pesa yao tumeelewana, tunataka mkandarasi aondoke akabidhi kazi yake bila madoa”alisema DC
 
Awali akina mama hao akiwemo Jenipher mbwilo mbele ya mkuu wa wilaya amesema kuwa walikuwa wakisomba mchanga kwa ajili ya ujenzi wa ghala hilo lakini mpaka sasa hawajamaliziwa madai yao.
“Tulikuwa tunasomba mchanga kwa hiyo hatujamaliziwa madai yetu tulikuwa wawili na mwenzangu mkandarasi bado hajatulipa”alisema Jenipher
 
Mwenyekiti wa kijiji hicho Abinel Mbilinyi amesema kuwa taarifa hizo anazo lakini inasemekana walidhulumiana kwani pesa yao ililipwa.

“swala hili ninalijua lakini hawa walikuwa na kiongozi wao na pesa hizo zililipwa sasa inasemekama walidhulumiana kwa hiyo inawezekana kiongozi wao ndio aliyewadhulumu,ila hili tatizo tulishalimaliza kwasababu tulikaa kwa maana kiongozi wao hawa atawalipa fedha”
 
Ghala ya kuhifadhia matunda lililokuwa likijengwa katika kijiji cha Madihani wilayani Makete limekabidhiwa kwa serikali likiwa limegharimu shilingi bilioni 1.1 hadi kukamilika kwake


Share.

About Author

Leave A Reply