Sunday, August 18

CHAMA CHA WENYE ULEMAVU WA NGOZI TANZANIA (TAS) CHALAANI VITENDO VYA UFUKUAJI MAKABURI

0


Na Amiri kilagalila

Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) nchini wamelaani vikali vitendo vya ufukuaji makaburi ya watu wenye ulemavu huo na kuondoka na masalia ya viungo vinavyofanyika Mkoani Mbeya na maeneo mengine nchini vinavyofanywa na baadhi ya watu ambao bado wanaendekeza mila potofu.

Akizungumza na vyombo vya Habari akiwa Mkoani Njombe Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania, Nemes Temba amesema vitendo hivyo vimekuwa vikiwaingiza kwenye hofu Kubwa na kukosa amani albino jambo ambalo linapingwa vikali huku wakiitaka serikali kuingilia kati ukomeshaji wa vitendo hivyo.

“Tunamwomba Rais John Pombe Magufuli kuingilia kati suala hili, ikiwa ni kutumia nafasi yake kukemea uovu huu na kuwezesha kifedha mikakati iliyopo na itakayokuwepo yenye nia ya kukomesha uovu huu dhidi ya Watu Wenye Ualbino na zaidi jamii ipate hamasa na kuziacha fikra potofu na matendo ya kishirikina,” ameeleza.

Ameendelea kwa kusema, “Jeshi la Polisi limefanya kazi nzuri na ya kupongezwa kwa kipindi cha miaka kadhaa iliyopita. Tunamsihi sana IGP Simon Sirro kuongeza kasi hasa katika upelelezi na kushiriki katika mchakato wa kuelimisha na kuhamasisha jamii kulinda na kuheshimu utu na uhuru wa Watu Wenye Ualbino na familia zao”.


Share.

About Author

Leave A Reply