Sunday, August 25

BODI YA LIGI YAFANYA MABADILIKO, AZAM NA YANGA

0


Na Shabani Rapwi

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imefanya mabadiliko ya uwanja katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) kati ya Azam FC na Yanga SC kutoka uwanja wa Taifa na sasa kuchezwa uwanja wa Uhuru Aprili 29, 2019 saa 10:00 jioni.

Kwa mujibu wa barua kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imeeleza kuwa mabadiliko hayo ya uwanja yanatokana na uwanja huo (Taifa) kutarajiwa kufungwa mara baada ya kumalizika kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, yakitarajia kumalizika Aprili 28, 2019 Jumapili hii nchini.


Share.

About Author

Leave A Reply