Saturday, August 24

AZAM FC YAIWASHIA MOTO MTIBWA SUGAR

0


Na Shabani Rapwi

Azam FC wameibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) uliopingwa Usiku wa Jana, May 22, 2019 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Magoli ya Azam yalifungwa na Donald Ngoma dakika ya kwanza ya mchezo na Enock Atta dakika ya 67.

Ushindi huo unawafanya Waoka mikate hao kufikisha alama 72 katika nafasi ya tatu wakiwa wamecheza michezo 35, wakishinda michezo 20, wakipoteza michezo 04 na wakitoa sale michezo 12 huku wakiwa wamesalia na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Yanga SC.

Pia Azam FC itakuwa na mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Lipuli FC, Jun, 02, 2019 katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.


Share.

About Author

Leave A Reply