Thursday, August 22

NAIBU WAZIRI MAVUNDE ALITAKA KANISA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI KWENYE UCHUMI WA VIWANDA

0


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde amewataka Wanataaluma na Wajasiriamali Wasabato(ATAPE) kushiriki katika uchumi wa Viwanda ili kuunga mkono Serikali chini ya Dr John Pombe Magufuli ambayo inaongozwa na falsafa ya “Uchumi wa Viwanda na Maendeleo ya Watu”.

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo jana Wilayani Bariadi,Simiyu wakati wa maadhimisho ya miaka 20 na ufunguzi wa Mkutano mkubwa wa wana ATAPE katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Kasekwa.

ATAPE mnao uwezo mkubwa wa kukusanya rasilimali zenu pamoja na mkashiriki kwenye uchumi wa Viwanda kwa lengo la kukuza Uchumi wa Taifa na pia kuongeza nafasi za Ajira hasa kwa Vijana.Nichukue fursa hii kuwaomba msiwe nyuma wakati wa Ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha Vifaa Tiba vitokanavyo na pamba hapa mkoani Simiyu ambapo zaidi ya Ajira 6000 zitatengenezwa kupitia uwekezaji huu”Alisema Mavunde

Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh Anthony Mtaka amewataka ATAPE kuhakikisha wanajiwekea malengo makubwa zaidi ili waweze kufanikiwa kiuchumi tofauti na ilivyo sasa ambapo bado kasi ya ukuaji wake kiuchumi ni mdogo kutokana na kushindwa kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi.

Naye Mwenyekiti wa ATAPE TANZANIA Ndg Freddy Manento ameahidi kuibadilisha Taasisi hii ili iendane na mahitaji ya dunia ya leo na kukuza mtaji wake kupitia uwekezaji mbalimbali wenye tija,kwa sasa ATAPE imefanya uwekezaji wa Tsh 1,200,000,000 katika sekta za kilimo na misitu.


Share.

About Author

Leave A Reply