Sunday, August 25

WAZIRI MKUU AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI WA AFYA NA WADAU WA AFYA JIJINI DAR ES SALAAM – Full Shangwe Blog

0


S

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (wakatikati) akiongozana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wakwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa mwisho kulia), wakiwa katika kikao cha kimataifa cha masuala ya Afya ambacho kimejumuisha nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini, kikao hicho kimefanyika jijini Dar es salaam.

DSC_0051

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia mbele ya Wadau wa masuala ya Afya wakiongozwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini katika mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya uliofunguliwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.

DSC_0075

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya, uliohudhuliwa na Mawaziri kutoka nchi za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini.

DSC_0105

Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na Wadau wa masuala ya Afya kutoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki, Afrika ya kati na Afrika ya Kusini wakati wa kikao cha kimataifa cha kujadili masuala ya Afya kilichofanyika jijini Dar es salaam.

DSC_0136

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimsalimia moja kati ya Wadau wa afya baada ya kumaliza kikao cha kimataifa cha kujadili masuala ya Afya kilichofanyika jijini Dar es salaam.

DSC_0153

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimtembeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika banda la Bohari ya Dawa (MSD) mda mchache baada ya kumalizika kwa Mkutano wa kimataifa wa masuala ya Afya uliofanyika jijini Dar es salaam.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.