Thursday, August 22

WANAWAKE CHANGAMKIENI FURSA ZA KIUCHUMI- DKT JINGU

0


1

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiendesha Mkutano wa wadau kujadili maendeleo ya Jinsia kutoka Taasisi, Wizara na baadhi ya Asasi za Kiraia uliofanyika leo Jijini Dodoma kushoto kwake ni Bi Hodan Addou Mwakilishi Mkazi Un Women Tanzania na kulia kwake ni Bw. Julius Mbilinyi Mkurigenzi Idara ya Jinsia Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeledo ya Jamii.

2

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Grace Mwangwa na Mkurugenzi wa watoto Bi. Mwajuma Magwiza wote kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii wakifuatilia kwa makini Mkutano Mkutano wa wadau kujadili maendeleo ya Jinsia katika Taasisi, Wizara na baadhi ya Asasi za Kiraia.

………………..

 

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wajumbe wa mkutano wa utekelezaji wa masuala ya kijinsia kuendeleza gurudumu la utekelezaji wa masuala ya Kijinsia ili kuhakikisha wanawake kote nchini wanaondokana na vikwazo vinavyowafanya wanawake wasishiriki katika kazi za maendeleo.

Dkt. John Jingu ameyasema hayo wakati wa kikao kazi cha siku moja Jijini Dodoma kilichowakutanisha wadau wa masuala ya Jinsia kutoka katika Wizara, Taasisi za Serikali na Wadau wa Maendeleo kinachokaa kujadili hali ya utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika Taasisi na baadhi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali.

Aidha Dkt. Jingu aliongeza kuwa bila kuondoa vikwazo vinavyokwamisha maendelo ya wanawake hapa Nchini itakuwa vugumu kufikia uchumi wa viwanda hivyo kuwataka wadau wa Mkutano kuhakikisha wanaweka wazi na kukomesha vikwazo vyote dhidi ya mwanamke ili kufikia uchumi wa viwanda.

‘’Hapa tunajadiliana kuhusu ni vitu gani vinavyowakwamisha wanawake lakini pia kupeana mrejesho wa nini kimefanyika kutoka kwa wadau na serikali kwa ujumla na kutoa matokeo ili kumsaidia mwanamke kumchangamkia fursa zilizopo za kujileta maendeleo.”Aliongeza Dkt. Jingu.

Aidha Dkt. Jingu amezitaja fursa zilizopo kuwa ni biashara na Masoko lakini pia teknolojia raisi zinazowawezesha wanawake kujiajili kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kama vile, vikapu, mekekeka na vifungashio vyinavyoongezea thamani biashara zao na kusisitiza kuwa lazima wanawake wachamngikie fursa ili zisije zikapotea.

Naye Mkurugenzi wa Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Julius Mbilinyi ameongeza kuwa suala la Jinsia ni suala mtambuka lakini pia akilihusianisha suala hilo na fursa za kilimo na viwanda akiongeza kuwa mkutano huu pia unaangazia nafasi ya mwanamke katika kilimo na maendeleo ya viwanda.

Aidha Bw. Mbilinyi aliongeza kuwa Mtazamo wa Mkutano huu ndio unatupa picha ya mtizamo wa Kijinsia katika kuleta mapinduzi ya viwanda akiangazia nyanja tofauti za kimaisha na kuzingatia mkutadha wa kijinsi kwa maendeleo endelevu.

Mkutano huu unaondelea Jijini Dodoma pamoja na mambo mengine unatoa fursa kwa wadau kutoa hali halisi ya utekelezaji wa masuala ya Kijinsia katika taasisi zao na hatua zilizofikiwa ikiwemo mrejesho wa nini kimefanyika na kuja na mapendekezo ya uondoshaji vikwazo vinavyokinzana na maendeleo ya wanawake.

 

Share.

About Author

Leave A Reply