Sunday, August 18

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUJIUNGA KATIKA VYAMA VYA KUTETEA HAKI ZAO NCHINI

0


vlcsnap-2019-04-30-06h05m58s155.png

Wafanyakazi wa umma , taasisi na makampuni nchini wametakiwa kujiunga katika vyama vya kutetea haki zao pindi wawapo kazini ili kupata mtetezi pindi haki zao zinapokiukwa na wa ajiri .

Katika siku za karibuni vyama kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi hususani walimu pamoja na wale wa kutoka makampuni binafsi wakidai kucheleweshwa kwa stahiki zao ikiwemo mishahara, upandishwaji wa maradaja na maengine mengi hatua ambayo wameitaja kuwa kikwazo kwa ustawi wa maisha ya familia zao.

Kufuatia changamoto hizo kuripotiwa na wafanyakazi hao katibu wa chama cha walimu CWT mkoa wa Njombe Fraten Kwahhison anawakumbusha wafanyakazi wanaokumbwa na mikasa ya udharirishaji na uvunjifu wa haki unaofanywa na waajiri pindi wawapo kazini kujiunga na vyama hivyo ili kupata msaada wa kisheria pindi wanapokutwa na changamoto hito.

Lakini licha ya siku hiyo kutambuliwa kiamataifa katika kuadhimisha siku ya mfanyakazi lakini suala la uelewa kwa wafanyakazi wengine limekuwa chini hatua ambayo inawafanya watu wengi kutokuwa kwenye vyama na kukumbana na changamoto kubwa pindi haki zao zinazopo vunjwa na waajiri. Baadhi ya wananchi wanatoa maoni kuelekea siku hiyo huku zaidi wakitaka vyama kujikita katika kudai haki za wanachama wao

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “
Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana wakati wa mishahara na masalahi bora kwa wafanyakazi ni sasa”ambapo katika mkoa wa Njombe itafanyika wilayani Wanging’ombe

 

Share.

About Author

Leave A Reply