Thursday, August 22

VIDEO:WATOTO WA KIKE MUWE CHACHU YA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA HASA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI: DKT NDUGULILE – Full Shangwe Blog

0


 

Pix 1

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (Mb) akiwasili katika Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga kuzindua Klabu za wasichana zitakazotumika kutoa elimu ya malezi na ujinsia kwa watoto wa kike kuhusu kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhdi ya watoto wa kike zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Pix 2 a

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga kuzindua Klabu za wasichana zitakazotumika kuwajengea uelewa watoto wa  kike kuhusu mbinu za kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Pix 3

Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’odi akitoa nasaha kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari ya Mwendakulima wakati wa uzinduzi wa Klabu za wasichana zitakazotumika kutoa elimu rika kwa watoto wa  kike kuhusu mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Pix 4

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkulu akitoa tamko thabiti kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile kuhusu azma ya Wilaya yake katika kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuendeleza juhudi za Serikali za Kutokomeza Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni pamoja na mimba na ndoa za utotoni.

Pix 5

Mwakilishi wa Klabu ya Wasichana katika Shule ya Sekondari Mwendakulima Anastazia Mabula (kushoto) akitoa taarifa yao kuhusu klabu za wasichana shuleni hapo wakati wa uzinduzi wa Klabu za wasichana zikazotumika kutoa elimu kwa watoto wa  kike kuhusu mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na mimba na ndoa za utotoni.

Pix 6

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akizungumza na wanafunzi wa  Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa  Klabu za wasichana zitakazotumika kutoa elimu kwa watoto wa kike kuhusu mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na mimba na ndoa za utotoni.

Pix 7 a

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile (hayupo pichani)  wakati wa uzinduzi wa  Klabu za wasichana katika Shule hiyo iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga zitazotumika kutoa elimu kwa watoto wa  kike kuhusu mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Pix 8

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua  Klabu za wasichana katika Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga zitakazotumika kutoa elimu na stadi kwa watoto wa  kike kuhusu kupambana na na vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Pix 9 a

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akitoa vyeti kwa baadhi ya wasichana walioshiriki mafunzo ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekindari Mwendakulima wakati wa hafla ya uzinduzi wa Klabu za wasichana katika Shule hiyo iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga zikazotumika kutoa elimu kwa watoto wa kike kuhusu mbinu za kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

Pix 10

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja akifurahia pamoja na baadhi ya mabinti walioshiriki mafunzo ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Mwendakulima waliohitimu mafunzo hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Klabu za wasichana katika Shule hiyo iliyopo Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga zitakazotumika kutoa elimu kwa watoto wa  kike kuhusu kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni.

 Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………

Watoto wa kike nchini wameaswa kujitambua, kujiamini na kujilinda dhidi ya vishawishi vinavyosababisha matukio maovu ya Ukatili wa Kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni na kusababisha kukatisha ndoto zao za kupata haki ya kuendelezwa na elimu bora kwa manufaa yao, family na Taifa.

Rai hiyo imetolewa na  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi wa klabu za wasichana katika shule ya Sekondari ya Mwendakulima.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinazidi kushamiri katika jamii zetu hususan katika meneo ambayo bado wanafuata mila na desturi ambazo zinamkandamiza mtoto wa kike na mwanamke.

Ameongeza kuwa namna bora ya kupambana na ukatili wa kijinsia ni kwa watoto wa kike kutonyamaza pale ambapo wanafanyiwa vitendo vya ukatili hasa kuozeshwa na kushawishiwa kuingia kwenye mahusiano ya kingono katika umri mdogo: mambo yanayosababisha mimba na ndoa za utotoni.

“Kila mtu aunge mkono juhudi zetu za pamoja za kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa kuacha usiri na kushirikiana kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia  kwa mamlaka zilizopo“ alisiistiza Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkulu amesema kuwa Wilaya yake inaendelea kushirikiana na jamii na wadau wa maendeleo katika kuendeleza juhudi za Serikali za Kupambana na Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni ili kuwapatia watoto wa kike haki yao ya kuendelezwa na kuwaandaa kuwa nguvu kazi bora ya Taifa la uchumi wa kati na wa viwanda.

Naye mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Mwajuma Salum amesema klabu za wasichana zinawasaidia sana watoto wa kike kujitambua kwa kupata elimu zinazowawezesha kupamabana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa mimba na ndoa za utotoni. 

Aidha, ameeleza kuwa mbinu wanazopata zinawasaidia kuishi na wanafunzi wenzao wa kiume kama kaka na dada wakiwa na jukumu la kuwalinda na kuwapa kuwashauri kuzingatia wajibu wao katika masomo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.