Tuesday, August 20

TOWNSHIP ROLLERS YACHAPWA NA AL-MERREIKHA LAKINI YASONGA MBELE,SASA KUCHEZA NA YANGA YA TANZANIA LIGI YA MABINGWA AFRIKA – Full Shangwe Blog

0


bostwana-1

Timu ya  Township Rollers kutoka botswana imesonga mbele katika hatua ya kwanza ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika licha ya kupokea kichapo cha 2-1 dhidi ya wenyeji Al Merreikh  mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Omdurman nchini Sudan.

Township Rollers wanasonga mbele kwa Jumla ya magoli 4-2 baada ya mchezo wa kwanza kuibuka na ushindi wa 3-0.

Kwa matokeo hayo Wabotswana hao watakutana na Mabingwa wa Watetezi wa Vodacom Tanzania bara timu ya Yanga ambayo nayo imesonga mbele kwa jumla ya magoli 2-1 dhidi ya St Luis ya Shelesheli

Mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kati ya marchi 5 au 6 mwaka huu  na mshindi wa hapo atatinga moja kwa moja kwenye hatua ya makundi na timu itakayotolewa hapo itaangukia kwenye Kombe la Shirikisho.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.