Tuesday, August 20

TANZANIA KUANZA KUWEKA ALAMA ZA KIMATAIFA KATIKA MIPAKA YAKE NA NCHI JIRANI ZA KENYA NA UGANDA – ANGELINA MABULA – Full Shangwe Blog

0


????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka baina ya Tanzania na Kenya kilichoharibika eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia alama ya kimataifa katika mpaka baina ya Tanzania na Kenya eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka baina ya Tanzania na Kenya eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga wakiangalia eneo la mpaka baina ya Tanzania na Kenya  eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia eneo la mpaka baina ya Tanzania na Kenya katika  eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia eneo la mpaka baina ya Tanzania na Kenya katika  eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga wakiwa katika picha ya pamoja na Askari  wa Kenya  wa hifadhi ya Masai Mara ambayo inapakana na hifadhi ya Serengeti wakati  alipokagua  mpaka baina ya Tanzania na Kenya  eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara.

????????????????????????????????????

Gari ya doria ya askari wa hifadhi ya Masai Mara  ya nchini Kenya  ambayo imepakana na hifadhi ya Serengeti  ikiwa katika msafara wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati wa kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya uliopo ndani ya hifadhi ya Serengeti.

????????????????????????????????????

Mto Mara uliopo katika hifadhi ya Serengeti Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.

………………

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula amesema Serikali itaanza kuweka alama za mipaka ya kimataifa katika mipaka yake na nchi jirani za Kenya na Uganda kuanzia machi mwaka huu.

Hatua hiyo inafuatia baadhi ya alama za mipaka yake na nchi jirani katika maeneo mbalimbali  kuharibika ama kuchezewa na hivyo kuleta mkanganyiko baina ya Tanzania  na nchi hizo  ni wapi mwisho wa mipaka.

Akizungumza katika ziara yake mkoani Mara, Mabula amesema kwa sasa fedha kwa ajili ya kazi hiyo imeshatengwa na kinachosubiriwa ni kuanza rasmi kwa kazi hiyo hapo machi mwaka 2018.

‘’katika zoezi la kuweka alama za mipaka vitawekwa vigingi kila baada ya umbali wa mita mia moja sambamba na kubainishwa eneo la ardhi huru’’ alisema Mabula.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, tayari timu ya wataalamu kutoka nchi za Kenya Uganda na Tanzania zimeshakutana na kukubaliana kuhusiana zoezi la uainishaji mipaka ya  nchi hizo.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  amesema kwa sasa alama zitawekwa katika mipaka iliyopo mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga na baadaye zoezi litaendelea katika maeneo mengine ya mipaka.

Amesema, ni imani yake baada ya kukamilika kwa zoezi la kuweka alama za kimataifa za mipaka suala la migogoro kuhusiana na mipaka litakwisha.

Kwa mara ya mwisho zoezi la kuweka alama za mipaka ya kimataifa baina ya Tanzania na nchi jirani lilifanyika mwaka 1975 baada ya lile la awali la Tangazo la Serikali (GN) mwaka 1965 kuhusiana na mipaka.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime Grorious Luoga alimueleza naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, mbali na suala la mipaka ya kimataifa wilaya yake inakabiliwa na changamoto ya mipaka baina ya hifadhi ya Serengeti na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo kwani wamekuwa wakivamia na kujenga ndani ya hifadhi na wakati mwingine kuingiza mifugo.

Katika ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika eneo la Serengeti, Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula alifuatana na Mkuu wa Wikaya ya Tarime Glorious Luoga pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Upimaji Vijijini kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Huruma Lugalla ambapo kwa pamoja walijionea hali halisi ya mpaka wa Tanzania na Kenya na baadhi ya alama za mipaka zilizoharibika.

 Read More

Share.

About Author

Comments are closed.