Sunday, August 18

TAIFA STARS YAPUNGUZA MAGOLI DHIDI YA ALGERIA MECHI YA KIMATAIFA YA KIRAFIKI,YAKULA 4-1 – Full Shangwe Blog

0


images

Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’imepunguza idadi ya magoli dhidi ya Algeria baada ya leo kufungwa magoli 4-1 Mchezo wa Kirafiki uliomalizika nchini Algeria
Carl Medjani amefunga moja, wakati mabao mengine yamefungwa na Baghdad Bounedjah mawili na Shomari Kapombe aliyejifunga.
Baghdad anayechezea Al Sadd ya Qatar alifunga bao la kwanza dakika ya 12akimalizia pasi ya Riyad Mahrez wa Leicester City ya England kabla ya kupsaua katikati ya mabeki wa Taifa Stars Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kudini na Kelvin Yondan wa Yanga Tanzania na kumchambua kipa, Abdulrahman Mohamed wa JKU ya Unguja.
Nahodha Mbwana Ally Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji akapiga shuti zuri dakika ya 14 baada ya pasi ya gardiel Michael Mbaga wa Yanga SC, lakini kipa Faouzi Chaouchi wa MC Alger  ya nyumbani akapangua kabla ya mabeki wake kuondosha kwenye eneo la hatari.
Zinedine Ferhat wa Le Havre ya Ufaransa alipiga fyongo dakika ya 18 baada ya pasi ya Baghdad ambaye naye alipasiwa na Salim Boukhanchouche wa JS Kabylie ya nyumbani.
Winga wa Difaa Hassan El – Jadidi ya Morocco, Simon Msuva akaifungia bao la kusawazisha Tanzania dakika ya 20 kwa kichwa cha kuparaza na mpira ukambabatiza Hillel El Arbi Soudani na kumpita kipa Faouzi Chaouchi kufuatia kona ya kiufundi ya winga wa Simba SC ya nyumbani, Shiza Kichuya.
Dakika moja kuelekea mapumziko, beki wa Simba SC, Shomari Kapombe akajifunga kwa kichwa kuipatia Algeria bao la pili dakika ya 44 akijaribu kuokoa krosi ya Sofiane Hanni.
Kipindi cha pili Taifa Stars walio chini ya kocha Salum Mayanga wakawa wepesi zaidi na kuruhusu mabao mawili zaidi, kwanza dakika ya 53 Carl Medjani akifunga kwa pasi ya Aissa Mandi kufuatia krosi ya Hillel El Arbi Soudani aliyepokea pasi ya Sofiane Hanni na baadaye Baghdad Bounedjah dakika ya 79 akiwachambua mabeki wote wa Stars na kukamilisha shangwe za mabao za The Green.
Taifa Stars ilizidiwa katika eneo la kiungo pamoja na kocha Salum Mayanga kupanga watu watatu, Mudathir Yahya wa Azam FC anayecheza kwa mkopo Singida United, zote za nyumbani, Said Ndemla wa Simba na Himid Mao wa Azam FC.
Baada ya mchezo huo dhidi ya Algeria, Taifa Stars inarejea nyumbani kucheza mchezo mwingine wa kirafiki Jumatatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.