Wednesday, August 21

TAIFA STARS YAIBINYA KONGO 2-0 UWANJA WA TAIFA MECHI YA KIMATAIFA YA KIRAFIKI – Full Shangwe Blog

0


29572496_575691096144006_1096070775909965058_n

Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeutumia vyema uwanja wa nyumbani baada ya kupata ushindi wa magoli mawili dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa kwenye uwanja Taifa Jijini Dar es salaam.

Kipindi cha pili timu zote zilikwenda bila ya kufungana kutokana na kushambuliana kwa zamu huku DRC walionesha kuliandama lango la Tanzania kwani vijana wa Mayanga walikuwa wakicheza kwa kujilinda

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko Ibrahim Ajib na Mudathiri Yahya walipoingia walibadilisha Mchezo na kuanza kushambulia kwa nguvu dakika ya 74 Mbwana Samatta aliwainua mashabiki wa soka kwa kufunga bao tamu kwa kichwa akimalizia krosi ya Kichuya kutoka upande wa kulia baada ya kazi nzuri ya Simon Msuva.
Kichuya akaifungia Tanzania bao la pili dakika ya 88 akimalizia pasi ya Samatta baada ya kazi nzuri ya winga wa Difaa Hassan El Jadidi ya Morocco, Simon Msuva.

Tanzania iliingia kwenye mchezo wa leo ikitoka kufungwa 4-1 na Algeria mjini Algiers Machi 22 katika mchezo mwingine wa kirafiki na kwa ujumla huu ni ushindi wa kwanza kwa Taifa Stars ndani ya mechi 10,

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Tanzania: Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Himid Mao/Mudathir Yahya dk73, Mohammed Issa ‘Banka’/Ibrahim Ajib dk59, Erasto Nyoni, Mbwana Samatta, Simon Msuva/Yahya Zayed dk90 na Shiza Kichuya/Rashid Mandawa dk87. 
DRC; Ley Matampi, Issam Mpeko, Glody Ngoda, Yannick Bangala, Wilfred Moke, Aaron Tshibola/Lema Mabibi dk46, Chancel Mbemba, Mubele Ndombe/Junior Kabananga dk54, Needkens Kebano, Bennick Afobe/Assombalanga Britt dk63 na Yannick Bolasie.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.