Thursday, August 22

RAIS DKT.MAGUFULI :ILI KUWEPO NA UCHUMI WA VIWANDA IMARA NI LAZIMA KUWA NA SEKTA YA AFYA ILIYO BORA – Full Shangwe Blog

0


2

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo mbele ya Viongozi wa Serikali na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati akizindua magari mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD) yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa tiba,

………………

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.

ILI kufikia katika uchumi wa kati kwa kutumia sekta ya viwanda Serikali inatakiwa kujikita katika kuimarisha sekta ya afya kwa watanzania ili kuwa na rasilimali watu wenye afya njema kwa ajili ya kuleta mafanikio hayo kupitia viwanda.

Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa magari 181 ya kusambazia dawa uliofanyika leo katika Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa (MSD) jijini Dar es salaam.

“Tunatakiwa kuwekeza kwenye uchumi wa Viwanda ili tufikie uchumi wa kati hivyo ni lazima tuwekeze kwenye sekta ya afya kwa kiwango kikubwa ili kuwa na wananchi wenye afya njema tayari kutumikia viwanda vyetu kwa muda wote” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania inatakiwa kujijengea viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini ili fedha zinazotumika kununua bidhaa hizo nje ya nchi zirudi mikononi kwa watanzania wenyewe pamoja na kutoa ajira kupitia viwanda hivyo.

Mbali na hayo Rais Magufuli amesema kuwa katika kuimarisha Sekta ya afya Serikali imetenga shilingi Bilioni 269 za kununua dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kutoka bilioni 31 katika bajeti ya fedha mwaka 2016/2017.

Kwa upande wake Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa katika kuimarisha Afya ya mama na Mtoto Serikali imepunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 60 kutoka asilimia 20 ya upunguzaji wa vifo hivyo.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa zina mgawanyo ikiwemo asilimia 42 zahanati na vituo vya afya ,asilimia 16 zinatumika kwa chanjo za watoto ,asilimia 10.2 zianenda hospitali za wilaya ,asilimia  6.8 zinatumia hospitali za mikoa ,asilimia 3.4 zinaenda hospitali maalum na asilimia 3 zinatumika kwa ajili ya dawa za saratani.

“Fedha hizo za dawa zipatazo Shilingi Bilioni 269 asilimia kubwa zinaenda kwenye vijiji na kata pamoja na zahanati na vituo vya afya na kufanya hali ya upatikanaji wa dawa kuwa juu mpaka kufikia hivi sasa” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa licha ya kuwa tu kuna upatikanaji dawa wa hali ya juu nchini lakini Serikali kupitia Wizara ya Afya imetengeneza muongozo wa matibabu kwa ajili  na kuwataka waganga wafawidhi wote nchini kutumia muongozo huo ili kutoa matibabu sahihi kwa wagonjwa .

Kwa mujibu wa Waziri ummy amesema kuwa katika kuimarisha sekta ya Afya nchini Serikali imejitahidi kuongeza huduma za matibabu ya kibingwa kwani hivi sasa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inapandikiza figo pamoja na vifaa vya usikivu kwa watoto ambapo imepelekea kupunguza rufaa za nje na kuokoa fedha nyingi.

Naye Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Dawa ya Taifa nchini (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa wanasambaza dawa za shilingi bilioni 18 kila mwezi na lengo ni kufikia bilioni 21 kufika mwezi julai mwaka huu.

Aidha Bw. Bwanakunu amesema kuwa mbali na upatikanaji wa dawa kuongezeka lakini kuna chanagamoto za maoteo kutoka ngazi ya zahanati kwani wanashindwa kujua mahitaji yao sahihi ya dawa zinazohitajika kwa mwaka hivyo kufanya MSD kushindwa kupeleka dawa kwa wakati.

Samabamba na uzinduzi huo wa magari  hayo 181 ya kusambazia dawa na vifaa tiba hapa nchini yaliyotolewa kwa ushirikiano wa Seikali ya Tanzania pamoja na Mfuko wa Dunia wa pamoja (Global Fund) pia Mhe. Rais Magufuli alipata kutembelea maghala ya dawa yaliyopo  MSD jijini Dar es salaam.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.