Sunday, August 18

PWANI KUTUMIA BIL. 5.6 KUKARABATI NA KUBORESHA VITUO VYA AFYA 13 -RC NDIKILO – Full Shangwe Blog

0


IMG-20180323-WA0023

Mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Yudas Ndungile, (wa kwanza Kushoto) akimueleza jambo mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo(mwenye shati jeupe) wakati alipofanya ziara ya kukagua vituo vya afya vya Kerege na Lugoba.

IMG-20180323-WA0022

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza na wananchi wakati alipokwenda kukagua vituo vya afya vya Kerege na Lugoba.

IMG-20180323-WA0021

Baadhi ya wananchi na viongozi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo (hayupo pichani)wakati alipokwenda kukagua vituo vya afya vya Kerege na Lugoba.

Picha na Mwamvua Mwinyi

…………………

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

 

MKOA wa Pwani unatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 5.6 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya 13 ili kuboresha utoaji huduma za afya,huduma za mama wajawazito na kupunguza vifo vya akinamama wakati wa kujifungua.

 

Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo wakati akikagua vituo vya afya vya Kerege na Lugoba,wilayani Bagamoyo.

 

Alieleza fedha hizo zinatolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye vituo hivyo vya afya ambavyo viko kwenye halmashauri za mkoa huo ikiwa ni fedha za awamu ya kwanza  ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo mei 31 mwaka huu.

 

Mhandisi Ndikilo alisema,awamu ya pili itakuwa ni kwa vituo sita na awamu ya tatu fedha zitatolewa kwa vituo sita kufanikisha ujenzi na ukarabati wa vituo hivyo .

 

“Fedha hizi zina umuhimu kwenye vituo hivi ,kwani serikali imedhamiria kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi hasa wakinamama ili wasipoteze maisha wakati wa kujifungua” alifafanua mhandisi Ndikilo.

 

Alielezea fedha hizo ni mpango wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk John Magufuli kuhakikisha huduma za afya zinaboreka kutokana ni nchi ya viwanda ili iweze kuwa na mafanikio na wananchi wake lazima wawe na afya njema.

 

Nae mganga mkuu wa mkoa wa Pwani Yudas Ndungile, alisema hadi sasa tayari zimeshatolewa kiasi cha sh. bilioni 3.5 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati .

Alisema baada ya kukamilika zitatolewa kiasi cha sh. milioni 220 kwa kila kituo kwa ajili ya vifaa tiba kwenye vituo hivyo ambapo kwa sasa ziko kwenye mchakato wa manunuzi.

 

Dk Ndungile alisema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya vituo vya afya ili kufanya ujenzi wajengo la maabara, chumba cha maiti, majengo ya upasuaji, jengo la akinamama na nyumba ya mtumishi.  

 

Akisoma taarifa ya kituo cha afya cha Kerege Mganga Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Sylvia Mamkwe alibainisha kituo hicho kimepewa kiasi cha sh. milioni 500 ambacho kiko kwenye hatua za umaliziaji.

 

Dk Mamkwe alisema, baadhi ya changamoto zilizojitokeza wakati wa ujenzi wa kituo hicho ikiwemo mvua kubwa iliyosababisha kubomoka kwa msingi na mafundi kuchelewesha ujenzi kwa wakati.

 

Naye mganga mkuu wa Halmashauri ya Chalinze ,Richard Machange alieleza wamepokea milioni 400 Kwa ajili ya kituo cha afya cha Lugoba  ambapo ujenzi unakaribia hatua ya linta.

 

Dk Machange alisema ,ujenzi huo wanawatumia mafundi wa kawaida ambao wamejenga kwa kiwango kizuri ambacho kina ubora kutokana na usimamizi wa halmashauri, wananchi ambao wameunda kamati maalumu ya ujenzi iliyoshirikisha makundi hayo.Read More

Share.

About Author

Comments are closed.