Tuesday, March 19

NSSF TPB KUENDELEZA MAHUSIANO MAZURI YA KIBIASHARA KWA TASISI HIZO

0


Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii, Dar es

Salaam

 

Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na
Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi wamekutana  leo jijini Dar es Salaam na kufanya
mazungumzo ili kuendeleza mahusiano mazuri ya kibiashara kwa Tasisi zao.

Wakuu wa
Taasisi hizo  walikutana katika ofisi ya
NSSF Makao  Makuu na walizungumza mambo
mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha
mahusiano ya biashara baina ya Taasisi hizo mbili ambazo zimekuwa
zikifanya huduma kwa muda mrefu.

Katika
mazungumzo hayo Mkurugenzi mkuu wa NSSF Ndugu William Erio alimuahidi
Mkurugenzi mtendji wa TPB aendelee kutarajia biashara yenye tija

Nae
Mkurugenzi mkuu wa TPB  Sebastia Moshingi
amesema  atawashawishi wastaafu wote wa
NSSF waliokuwa wakilipwa pensheni zao kupitia Shirika la Posta wafungue Akaunti
TPB ili waweze kufaidika na huduma mpya ya kulipa wastaafu wa NSSF ambapo
mstaafu atalipwa pensheni yake moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Benki hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi  wakiwa katika picha ya pamoja na kupeana mikono mara baad aya kumalizika kwa mazungumzo ya ushirikiano w ahuduma baina ya Tasisi wanazoziongoza

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi  pamoja na watendaji wamashirika yote mawili wakiwa katika kikao cha kujadili huduma watakazoshirikiana.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndugu Willam Erio  na Mtendaji Mkuu wa TPB Ndugu Sabasaba Moshingi  wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mashirika wanayo yaongoza.Check Also1

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. …

Share.

About Author

Leave A Reply