Monday, March 25

NAIBU WAZIRI MAJI MHE. JUMAA AWSEO AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI LINDI; AKABIDHI MRADI WA MAJI WA CHIKONGE KWA MAMALAKA YA MAJI LINDI

0


 

Na. Athumani Shariff – Lindi

Naibu wa Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) leo ameanza ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maji katika mkoa wa Lindi kwa kutembelea na kutolea maagizo katika miradi ya Ng’apa, kimeng’ene, chikonji,

Akiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Lindi, alipokea taarifa ya sekta ya maji ya mkoa wa Lindi iliyomwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Ndemanga kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa safarini.

1. NAIBU WAZIRI- MAJI JUMAA AWESO AKIKAGUA MAJI KWENYE MITAMBO YA KUTIBU MAJI NG'APA LINDI-min

Aidha katika mradi wa maji wa Ng’apa unaohudumia Manispaa ya Lindi Mheshimiwa Aweso aliihakikishia menejimenti na bodi ya LUWASA kuwa atasimamia upatikanaji wa fedha kwaajili ya kuongeza mtandao kwa maeneo ambayo hayana mtandao kwa kiasi cha kilomita 40 kama ilivyo kwenye bajeti ya 2018/19. Pia aliwataka watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Lindi (LUWASA) wahakikishe wanajipanga kwa kutumia mapato ya ndani ili kuongeza mtandao wa maji ili waongeze kipato.

Pia aligiza Wizara ya Maji kushughulikia swala la marekebisho ya busta iliyoharibika na visima 3 katika mradi huo, kwani mradi huo unaendeshwa kwa busta 2, lakini kutokana na hitilafu busta 1 imeharibika na sasa inayofanya kazi ni busta 1. “Naagiza busta hii irekebishwe haraka kwakuwa busta inayofanya kazi sasa ni moja nayo ikiharibika mji wa Lindi utakosa maji kabisa”. Alisema.

5. NAIBU WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AKITOA MAAGIZO KWA KAMPUNI NA MAMLAKA JUU YA HAKI ZA WALINZI WA KWENYE VISIMA VYA MAJI NG'APA LINDI.-min

Akiongea na wakazi wa kijiji cha Kimeng’ene Kwenye mkutano wa hadhara alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inatekeleza ahadi zake kwa vitendo na imedhamiria kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa kumsogezea huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza karibu na makazi.

3. NAIBU WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AKIPANDA KWENYE TANK LA MAJI NG'APA LINDI-min

Katika mradi wa Kimeng’ene unaotumia nishati ya umeme wa dizeli, Mheshimiwa Aweso alilazimika kuongea na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Kalimani ili kuwezesha mradi huo kutumia nishati ya umeme wa REA kwani ni umbali wa kilimomita 2 tu kutoka kwenye nguzo za umeme hadi kwenye mradi, jambo amabalo wananchi walitakiwa kuchanga asilimia 18 ya gharama za kupeleka umeme kwenye mradi kiasi ambacho tayari walishakitimiza.

2. NAIBU WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AKIHAKIKI MITA YA MAJI KWENYE MRADI WA MAJI WA CHIKONGE - LINDI-min

Mheshimiwa Aweso ataendelea na ziara katika miji ya Ruhangwa, Nachingwea, Liwale na Kilwa na baadae atatembelea chanzo cha maji cha Matema Wilayani Newala.

Share.

About Author

Leave A Reply