Tuesday, March 19

MNZAVA: WAKULIMA,WAFUGAJI ONDOENI UBINAFSI

0


IMG_8309

MBUNGE wa korogwe vijijini Mh Timotheo Mnzava amewataka wananchi jamii ya wafugaji na wakulima waishio katika kata ya Mkalamo na Magamba Kwalukonge kumaliza tofauti zao na kuachana na ugomvi baina yao na malumbano yasio na tija ili kuleta maendeleo ya kata zao na Korogwe na taifa kwa ujumla.

Ameyazungumza hayo leo katika mikutano yake na wananchi hao alipotembelea katika kata hizo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukutana na wananchi ambapo lengo kuu ni kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo.

Mnzava amezitaka jamii zote mbili za wafugaji na wakulima kuondoa ubinafsi katika mioyo yao na kwa  pamoja wawe na upendo baina yao na kuishi kindugu ili kulinda amani ambayo ni tunu kwa taifa la Tanzania.

Natambua changamoto yetu ya Ardhi, na naamini hata siku moja hatuwezi kufuta mashamba yote, kwasababu uwekezaji pia tunauhitaji lakini uwekezaji wenye tija, lakini hata ikitokea siku moja mashamba yote tukapewa kama hatuna matumizi bora ya ardhi, kama hatutaacha ubinafsi na kuchukiana, mgogoro wa wakulima na wafugaji hauwezi kwisha. Tupendane, tuishi kama ndugu na kuheshimu shughuli za wenzetu”. Alisema Mnzava

Mnzava amewaahidi wananchi hao kuendelea kuwasemea juu ya tatizo la uhaba wa Ardhi na amewaomba wavute subira kwani serikali ya Rais Magufuli inalifahamu tatizo hilo na kwakuwa Rais anawajali watu wake litapata suluhisho.

Share.

About Author

Leave A Reply